| Mwinjilisti Nazery akihubiri mahubiri ya tarumbeta ya vitabu katika viwanja vya shule ya msingi Mavurunza- Kimara Dar Es Salaam yakiletwa na kanisa la Kimara sda. |
Mahubiri ya sherehe za utume ya Extravaganza yanayoendelea ikiwa ni wiki ya tatu sasa,katika mkutano unaoendeshwa na wainjilisti toka kanisa la Kimara mkutano huu umebariki wengi ikiwa na makadilio ya wastani wa watu 70 wageni wasio wa imani kuja kusikiliza mahubiri hayo.
Injilileo ilipata fursa ya kufanya mahojiano na mwinjilisti Godfrey Nazery ambaye ni mshiriki wa kanisa la waadventista wasabato na amekuwa akifundisha masomo ya mahusiano juu ya imani mbili yaani ya waislamu na wakristo kwa kutazama vitabu vya biblia na Quran.
Mwinjilisti alisema kuwa mpasuko haupo baina ya waumini wa dini hizi mbili sema tu shetani ndio amepumbaza watu kuwa sisi tuna mpasuko wakati sisi hatuna mpasuko.
Mwinjilisti Nazery alisema.."Kiukweli namshukuru Mungu imeonekana hiyo na watu wameweza kuelewa kwamba hakuna mpasuko cha msingi ni kuonesha ya kwamba ibilisi ndiye kikwazo katika maisha yetu lakini kiukweli mpasuko haupo baina ya imani"
Pata kusikiliza mahubiri haya ujue mengi juu ya mahusiano dhabiti kwa imani hizi mbili hapa SIKILIZA HAPA
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***



0 comments:
Post a Comment