Afisa
Mtendaji Mkuu Dr Kamugisha Kazaura atembelea mikoa ya Lindi, Mtwara,
Ruvuma na Mbeya ikiwa na lengo la kukagua miundombinu ya TTCL na Mkongo
wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TTCL wa
mikoa hiyo.
Dr
Kazaura ailijionea juhudi mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa TTCL
katika kuhakikisha miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano inakuwa salama muda.
Hivi
sasa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imekuwa kampuni pekee ya
mawasiliano ambayo imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali kupitia
mtandao wake.
Wateja
hao ni pamoja na TAMISEMI, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya
Bandari Tanzania(TPA), Mabenki, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali
(CAG),Wizara ya Fedha, watoa huduma za mtandao/intaneti (ISPs) pamoja
Makampuni ya Simu
Pia
TTCL imefanikiwa kuunganisha nchi jirani katika ukanda huu wa afrika
Mashariki (Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda) pamoja na nchi za kusini wa
Jangwa la Sahara (SADC) ambazo ni Malawi na Zambia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua mitambo ya TTCL mkoani Lindi.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akipokea maelezo kutoka kwa
wafanyakazi wa TTCL Mtwara kuhusu juhudi zinazofanyika kulinda na
kusimamia mitambo yake.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua Mtambo wa Mkongo wa Taifa,
pembeni yake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi wa TTCL,Senzige Kisenge
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na mafundi ambao wanajenga
Barabara katika mkoa wa Ruvuma, akiwasisitiza walinde Mkongo wa Taifa.
Meneja
wa TTCL mkoa wa Lindi- John Nindwa akimuonesha Afisa Mtendaji Mkuu wa
TTCL, Dr Kazaura eneo ambalo Mkongo wa Taifa ulikatwa na wezi katika
hifadhi za Taifa ya Selous na juhudi zilizofanyika katika kurejesha
mawasiliano Ruvuma.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na wafanyakazi wa TTCL
mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi Senzige Kisenge na
Kushoto Mkuu wa Biashara Nyanda za juu Kusini, Juvenal Utafu.
Hii ni
baadhi ya maeneo ambayo awali Mkongo wa Taifa ulikatika kutokana na
mmomonyoko wa ardhi, lakini TTCL ilihakikisha inapitissha Mkongo juu
kwenye nguzo za Simu ili kurejesha mawasiliano.
Wafanyakazi
wa TTCL wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura
wakiangalia eneo ambalo Mkongo wa Taifa ulikatika mkoani Njombe
kutokana na mmomonyoko wa ardhi , lakini juhudi zilifanyika usiku na
mchana kuhakikisha mawasiliano yanarejea katika hali yake ya kawaida.
Hali
halisi ya mmomonyoko wa ardhi uliosababishwa na mvua kubwa ailionyesha
Mkoani Njombe na kusababisha Mkongo wa Taifa kukatika.
JPG
Wafanyakazi wa TTCL Mbeya wakiwa katika mkutano ambao uliitishwa Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kazaura ikiwa ni sehemu ya kuzungumza na
wafanyakazi wake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na wafanyakazi wa TTCL mkoani Mbeya.
Dr
Kazaura akizungumza na Afisa wa Malawi baada ya kutembelea Mkongo wa
Taifa eneo la Kasumulo mpakani kati ya Tanzania na Malawi.
Kaimu
Meneja Mkoani Mtwara Kilango Bakari akieleza juhudi zinazofanywa na TTCL
katika kutoa huduma kwa wateja wake mkoani Mtwara.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na wafanyakazi wa TTCL
mkoani Lindi. Aliyesimama ni Mkuu Biashara Kanda ya Kusini Hussein Nguvu
akieleza juhudi zinazofanywa na Mkoa katika kusimamia mkongo na
shughuli za TTCL kwa ujumla.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)


0 comments:
Post a Comment