Sunday, February 15, 2015



Morning Start Television imeandaa tuzo zitakazoitwa Groove Music Award. Katika awamu ya kwanza, zoezi hili litafanyika mkoa wa Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Wakurugenzi wa Vijana na Muziki wa Konferensi za SET na SEC ambao pamoja na Mkurugenzi wa Vijana na Muziki wa Union wataunda kamati ya majaji. Jopo hili la watu watatu litapendekeza kwa MSTV majina mengine matatu ya wataalamu (ambao si wachungaji) wanaoweza kuwepo wakati wa kurekodi kipindi kuanzia March 2015.
Zoezi la usajili wa wa waimbaji litaanza tarehe 17 Februari, 2015 na kufungwa tarehe 17 Machi, 2015, kisha kufuatiwa na usaili na kisha kufunguliwa kwa watazamaji. Fomu ya usajili yenye masharti na utaratibu wa kujiunga/kushiriki imeandaliwa ambapo kila mwombaji atapewa kwa kulipia gharama kidogo ya Tshs. 5,000/= katika makao makuu ya MSTV au kupitia Bank ya NBC. AC No 02210300650, jina la Akaunti MORNING STAR RADIO..
Fomu za usajili zinapatikana Makao makuu ya MSTV AU maombi kupitia
grooves@morningstartv.or.tz. Kila mwombaji atatakiwa kuchagua kipengere ambacho angependa kushiriki kati ya vipengere 11 vivilivyopo kama ifuatavyo:

A. Kwaya ya mwaka.
B. Kikundi cha watu watatu/zaidi cha mwaka (trio, quartet, quintet,
C. double quartet).
D. Waimbaji wawili bora zaidi (Best duet).
E. Mtunzi mahiri wa mwaka (Ujumbe, sauti, mpangilio, utamu wa wimbo).
G. Mpangaji muziki mahiri wa mwaka (Music arranger of the year).
H. Kwaya ya watoto ya mwaka.
I. Mwanamuziki wa kiume wa mwaka.
J. Mwanamuziki wa kike wa mwaka.
K. Mwanamuziki wa kiume anayeibukia.
L. Mwanamuziki wa kike anayeibukia.
M. Kundi linaloibukia (trio, quartet, quintet, double quartet).
Mungu awabariki mnapopanga kushiriki kipindi hiki cha kwanza na cha pekee kupitia Luninga yako uipendayo ya Morning Star TV.
IMETOLEWA NA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA UNION YA KUSINI MWA TANZANIA

 Habari na Mazara Matucha
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA