Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la
Mitihani nchini (NECTA), Dk.Charles Msonde amesema katika matokeo ya
kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu umeongezeka kwa asilimia
12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Katika matokeo hayo msichana wa shule ya
sekondari ya Baobab, Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na
kufatia wavulana.
Shule za Sekondari za St.Fransis ya mkoani
Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo
kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na
shule zingine.
Msonde amasema matokeo hayo yanatokana na mfumo mpya wa GPA kwa kuangalia masomo saba hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.



0 comments:
Post a Comment