Vurugu zilizofanywa na baadhi ya
walemavu wa ngozi Albino katika Ikulu ya Tanzania zimesababisha
kuahirishwa kwa kikao kati ya viongozi wao na Rais Jakaya Kikwete.
Rais
Kikwete alikuwa akitarajiwa kufanya mkutano na viongozi wa Albino
Tanzania TAS aliowaalika kuzungumzia hoja zao kutokana na mauaji ya
walemavu hao yanayoendelea nchini humo.
Lakini heka heka iliyotokea katika eneo la mapokezi iliwalazimu maafisa wa Ikulu kuwatawanya walemavu hao.
Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania wakiwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, |
Kelele hizo na mabishano
hayo miongoni mwa walemavu hao kwa mbali ikaanza kuonekana ni dosari
namba moja hasa baada ya kupandisha mori na kila mtu kuanza kusema lake
kupinga ushiriki wa viongozi hao
Kutokana na vurugu hizo maafisa
wa Ikulu waliwatawanya Walemavu hao kutoka nje ya Geti , na hapo ikawa
mwanzo wa sakata jipya baada ya kuanza kulumbana na viongozi wao na
hatimaye kuanza kupigana na mambo yakawa hivi.Baada ya kutulizwa ugomvi
kilichofuata ni nyimbo za kupinga uhalali wa viongozi wao
Hata
hivyi vurugu hizi zinatazamwa tofauti na baadhi ya walemavu hao,ambao
wanasema ni vurugu hizo zimepoteza fursa ya kuwasilisha matatizo yao
kwa Rais
0 comments:
Post a Comment