Ufunuo wa Yohana 19:13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu
Yohana 17:17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli
Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli
Kukataa maneno ya Mungu ni kumkataa kristo,ni kukosa utakaso,Yeye ndiye amekuwa akizungumza na watu katika vizazi vyote,wamekuwepo watu mashujaa na waaminifu waliolipokea neno la Mungu kwa uaminifu kwamba yalikuwa mema machoni pao au la walitii.
Yeremia 42: 5 Wakamwambia Yeremia, Bwana na awe shahidi wa kweli na uaminifu kati yetu; ikiwa hatufanyi sawasawa na neno lile, ambalo Bwana, Mungu wako, atakutuma utuletee.
6 Likiwa jema, au likiwa baya, sisi tutaitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake; ipate kuwa faida yetu, tunapoitii sauti ya Bwana, Mungu wetu.
Matendo ya Mitume 17:11 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
Zaburi 53:2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu
Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
Wewe ni miongoni mwa watu wengi,wenye akili,ambao wana sema wewe Yesu ambaye umesema na watu wote katika vizazi vyote,ninahitaji kuwa na roho waliyokuwa nayo waberoya,nilisome neno,nikakutii mwokozi,mimi ni wa kwanza maana ninahitaji kuyasikia maneno ya Yesu,unaweza ukamwambia YESU usinipite unapotafuta watu wenye akili wanaosikiliza neno lako ulipo,Bwana akubariki. Ombi Bwana na Muumaji wa Vyote,asante kwa fursa ya hii uliyompatia msomaji. Maisha yake ameyatoa kwako ili awe miongoni mwa wengi wenye akili wakutafutao wewe, onekana kwake sasa na hata milele katika jina la Yesu Kriso lenye nguvu amen
0 comments:
Post a Comment