Na Andrew Chale wa modewji blog
Dk.
Ally Possi ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.
Akielezea na kuchambua kwa kina kuhusiana na wimbi la mateso na mauaji
dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wenye albinism.
Mo dewjiblog,
iliamua kufanya mahojiano maalum ilikukuletea wewe msomaji wetu
unayeperuzi mtandao wako bora kabisa kujua na kuelewa na nini kifanyike
ikiwemo mimi na wewe katika kuchukua hatua.
Suala la mauaji dhidi ya watu wenye albinism:
“JAMII
yenye ushirikina ndio yenye kuamini suala la mauaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi ambao wana albinism, hivyo ilikuondoa imani hii potofu
ni kutoa elimu katika maeneo yote na kuwalinda popote pale, Jambo hili
ni jukumu letu sote” anabainisha Dk. Ally Possi.
Dkt.
Possi anabainisha kuwa, Serikali itaendelea kulaumiwa mpaka hapo juhudi
za dhati za kukomesha mauaji na vitendo vya kikatili vitakavyochukuliwa
na kutokomezwa kabisa.
Fuatilia hapa Mahojiano hayo maalum.
Mwanasheria na mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dk. Ally Possi akiwa kwenye ofisi za modewjiblog kabla ya mahojiano na mtandao huu.
MO DEWJI BLOG : Karibu,
mgeni wetu katika mtandao huu wa kijamii unaokuletea habari bora kabisa
zilizochambuliwa kwa kina za ndani, nje na makala maalum za kina.
DK. POSSI: Asante, nashukuru sana…
MO DEWJI BLOG: Unadhani nini chanzo na hali ya ongezeko la vitendo hivi kwa sasa hapa Tanzania?
DK.POSSI: “Kwanza mauaji ni.. yanatokana na imani potofu. Imani potofu kwa jamii kuwa ukipata kiungo cha alibino unafanikiwa.
Hii ni imani potofu kwa jamii ya watu wenye kuamini ushirikina.
“Albino ni ulemavu ambao mtu anakosa aina ya vitamin inayoitwa melaniani…
Inakosekana
ikiwemo katika ngozi, nywele na macho” anaendelea kubainisha kuwa: Kuwa
albinism ni hali ya kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili ama mmoja. Ni
kwamba baba na mama wanakuwa na vinasaba vinavyokuwa na albinism na
vinapokutana wakati wa kutunga mtoto ndipo mtoto mwenye albinism
anazaliwa.
MO DEWJI BLOG: Vipi inahusishwa na suala la Imani?
DK. POSSI: “Imani sio dini, Ni imani ya kishirikina.
“Sijui
kitu gani ambacho kimetokea kikaleta hiyo imani, kwa kifupi ipo kwenye
jamii iliyoendelea na uwezo wake wa kiuchumi ni mdogo na elimu pia.
Pia
tunaweza kusema: “Suala hili ni la imani, Imani si ya dini, bali ni ya
kishirikina. Kwa sababu kuna mtu anasema yeye muislamu ama mkristo.
Au
kuna mtu ana Phd/ Profesa, ama amesoma elimu nzuri tu ama ana pesa
anafanya biashara au mfanyabishara au mwanasiasa mwenye elimu yake nzuri
lakini ametumbukia kwenye imani hii ya kishirikina.
Mwanadishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale akiwa kwenye mahojiano maalum na Dk. Ally Possi.
MO DEWJI BLOG: Kwa nini Kanda ya ziwa mauaji haya yamezidi kwa kasi?.
Dk. POSSI: “Kwanza kuna tatizo: Ofkozi..mauaji hayo Kanda ya ziwa mauaji yameripotiwa sana pia kuna Morogoro pia na sehemu nyingine.
“Serikali
imekuwa kimya sana… katika mauaji yametokea husikii kiongozi mkubwa,
ukiondoa Rais alivyosema (Machi 2-wakati wa hotuba ya mwisho wa mwezi wa
Februari), lakini kiongozi mkubwa wa juu Waziri Mkuu, tangu mtoto
Yohana yule wa Geita, Chato kukutwa ameuwawa
Sijasikia kauli nyingine zaidi ya Rais…Ambayo nayo ameitoa wiki mbili hadi moja na nusu, kupita ndio Rais anatoa tamko hilo.
“Nafikiri
Serikali imekaa kimya kutoa matamko ama imekuwa ‘slow’ kuchukua
maamuzi ama hatua stahiki hasa kwa watuhumiwa huko vijijini.
“Sote
tumekaa vijijini ama tuna ndugu vijijini, Mtu anaweza kuibaa Baiskeli
kijijini lakini masaa tu, anakamatwa. Lakini watuhumiwa wale wa vijiji
wa mauaji ya watu wenye albinism kwa nini ichukue muda wasikamatwe?.
MO DEWJI BLOG: Tuambie inakuaje katika suala la kisheria?.
Dk. POSSI:
“Sidhani kama kuna kitu kigumu kuwachukua watuhumiwa vijijini, wakati
mtu akiiba baiskeli baada ya muda anakamatwa. Hapa nadhani suala la
kisheria lipo kwa watu wote. Sheria inabidi ichukue mkondo wake kwa
kuchukua maamuzi stahiki na ya haraka katika kuyafanyia kazi ikiwemo
kuwakamata watuhumiwa popote walipo.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment