Friday, March 06, 2015

Rais wa zamani wa Ghana John Kufour
Tume ya kudumu ya waangalizi wa uchaguzi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imerejea Nigeria kufatilia uchaguzi wa nchi hiyo uliopangwa tena kufanyika Machi 28 na Aprili 11.
Timu hiyo ambayo ni sehemu ya wajumbe 250 wa tume ya ECOWAS inaongozwa na rais wa zamani wa Ghana John Kuffor.
Wajumbe wengine 18 wa timu hiyo wanatarajiwa kuwasili nchini humo wiki ijayo.
Awali waangalizi hao walipelekwa kwenye majimbo sita ya kisiasa mwezi Januari na kuondoka nchini humo kufuatia kubadilishwa kwa tarehe ya uchaguzi.
Mwanzoni uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Februari 14 na 28 lakini ulibadili tarehe ilibadilishwa baada ya ushauri kutoka kwa mshauri wa mambo ya usalama wa taifa Sambo Dasuki na wakuu wa jeshi ambao hawakuwa na uhakika na usalama wa uchaguzi huo.
 

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA