Kongamano la
uimbaji mkoa rukwa la fanyika kwaajili ya kuinua kiwango cha muziki pamoja na
kuhifadhi nyimbo katika mfumo wa picha, idara ya muziki kwa kushirikiana na idara ya mawasiliano -shc wameendesha kongamano
huko kanisala waadventista wa sabato kantalamba lililoko mjini sumbawanga
mkoani rukwa nakuhudhuriwa na kwaya 28 kutoka pande zote za mkoa wa rukwa. kila
kwaya iliimba nyimbo nne(nyimbo 2 za chaguo lao na wimbo namba 25&8 ktk
kitabu kidogo cha nyimbo za kristo)
Katika utaratibu
huu uliyo anzia mpanda mkoa katavi na hatimaye sumbawanga mkoani rukwa pia
utafanyika mbinga mkoani ruvuma, mafinga mkoani iringa(mkoa njombe pia
utahusika hapa) na jijini mbeya mkoani mbeya unaambatana na kutoa asilimia ya
uwezo wa kila kwaya ili kuleta hamasa ya kuongeza juhudi ya kujifunza muziki na
kupata kwaya 10 za shc zitakazo kusanyishwa mbeya kwaajili ya kurekodiwa na
morning star tv.Aidha mch.D. Bambaganya
amewataka waimbaji wa mkoa katavi na rukwa kuinua viwango vyao vya muziki kwa
kutafuta wataalamu wa muziki na kufanya makongamano ya kimtaa mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment