Mchungaji mwakalonge akiongelea juu ya kua kiongozi bora na kanuni zak |
1. Jiepushe na mgongano wa maslahi.
2. Uwe kiongozi na siyo mfia dini. Ujue kuchukuliana bila kushuka Viwango vyako.
3. Hamasisha watu kwa kuonesha kuwa unawajali
4. Jenga viongozi usiwakate miguu
5. Usiweke watu wote wenye uwezo kwenye nafasi ya Uzee wa Kanisa na kuacha idara bila watu makini
6. Usikurupukie mashitaka ya viongozi bila kuyafanyia utafiti
7. Ita vikao kwa wakati kwa mujibu wa Mwongozo wa Kanisa
8. Kuza stadi za kutawala vikao
9. Mtu mmoja asitawale mijadala
10. Fahamu muda muafaka wa kupiga kura
11. Kamwe usipigie kura yaliyofafanuliwa na sera za Kanisa na Mwongozo wa Kanisa
12. Usifanye kazi ya kumwogopa au kumfurahisha mtu
13. TUMIA MATHAYO 18 kumsaidia mkosaji
14 Weka Makengo makubwa ya kupanga makanisa
15. Shirikiana na Uongozi wa juu usipingane nao
16. Mchungaji wa mtaa anapaswa kuwa muidhinishaji wa pesa zote za Kanisa
17. Omba msaada na mashauri kutoka ngazi za juu.
18. Himiza maendeleo ya kazi ya Kanisa ulimwenguni mwote. Usiione kazi katika Kanisa mahalia kuwa muhimu kuliko kwingineko.
19. Himiza matukio yaliyo kwenye kalenda na mahitaji ya taasisi za Kanisa
20. Tumia uangalifu kuanzisha miradi mikubwa inayozidi Uwezo wa washiriki
21. Tekeleza kwa uaminifu 'Azimio la Iringa'
22. Hakikisha una vifaa vya kutosha na vinavyokidhi afya na staha vya meza ya Bwana na Ubatizo
23. Elekeza utaratibu unaofaa wa kuwahudumia wanaobatizwa na wabatizaji
24. Utambulisho uwe mfupi unaozingatia mambo muhimu na kutaja kwa usahihi majina ya watu
25. Usitumie Mali, muda, na raslimali watu wa ofisi kwa matumizi binafsi
26. Magari ya kiofisi yatumike kwa shughuli za kiofisi tu
Haya yamesemwa leo na Mchungaji Mwakalonge - Mwenyekiti wa Union Misheni ya Kusini mwa Tanzania kwenye semina ya Viongozi inayohitimishwa leo hapa Morogoro.
0 comments:
Post a Comment