Raisi wa Tanzania Jakaya Mrisho na Uhuru Kenyata wakizungumza |
Katika makubaliano hayo ndege za Kenya Airways sasa zitafanya safari zake kama kawaida nchini Tanzania na magari ya Tanzaniayataruhusiwa kuchukua watalii na abiria katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.Kutoka pia Waziri wa Mambo ya nje Bwana Bernald Membe amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya viongozi hao wakuu wanchi hizo mbili kukutana nchini Namibia walikokwenda kuhudhuria maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Namibia na kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo.
Awali kabla ya uamuzi wa marais hao, magari ya Tanzania yaliyokuwa yakichukua watalii katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta,
yalipigwa marufuku na serikali ya Kenya katika agizo lililotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki,
Kenya Airways zinazoingia Tanzania kupunguza safari kutoka 42 kwa wiki hadi 14 pekee.
Makubaliano ya marais hao yanakuja siku chache baada ya mzungumzo ya mawaziri wa utalii wa Tanzania na Kenya kuvunjika mwishoni mwa wiki
kufuatia pande hizo mbili kushindwa kufikia muafaka kuhusu magari ya Tanzania yaliyopigwa marufuku uwanja wa Jomo Kenyatta.Huku pia mamlaka ya anga ya Tanzania na ile ya Kenya nazo zikishindwa kufikia muafaka kuhusu kupunguza safari za ndege za kenya zinazoingia Tanzania.
0 comments:
Post a Comment