dunia akiwa |
Waziri mkuu mwanzilishi wa Singapore, Lee Kuan Yew amefariki dunia.
Lee amefariki akiwa na umri wa miaka tisini na mmoja kutokana na ugonjwa wa mapafu.Kwa miongo mitatu ya utawala wa Lee alifanikiwa kuipitisha nchi yake katika kipindi cha mpito na kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo walizokuwa nazo na sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara cha kimataifa.
David Adelman ni balozi wa zamani wa Marekani nchini humo, ametuma salamu zake za rambi rambi.
Lee ni mwanamume mwenye nguvu ya ushawishi aliyeingia madarakani katikati ya miaka ya sitini .Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani ambao umedumu hata leo
Yew aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 91 baada ya kuugua homa ya mapafu.Nchini Uchina, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imemsifia na kumtaja Lee Kuan Yew, kama kiongozi wa kipekee wa bara Asia.
Marehemu Lee ambaye aliiletea mabadiliko makubwa taifa la Singapore na kuwa na mojawepo ya bandari maarufu zaidi Duniani huku uchumi wa nchi hiyo ukiimarika maradufu, atasalia katika kumbukumbu la taifa hilo.
Mwanawe ambaye ni waziri mkuu wa sasa nchini humo, Lee Hsien Loong, anasema kuwa Singapore haitawahi kuwa na mtu kama huyo tena.
Naye waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, anasema kuwa Bwana Lee alikuwa mmojawepo wa viongozi wakuu duniani.Serikali ya Singapore imetangaza siku sita ya maombolezo, hadi atakapozikwa siku ya Jumapili.
0 comments:
Post a Comment