Ugunduzi huo uliofanyika nchini
Ethiopia unasema kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yaliathiri maumbile ya
binaadamu aliyetegemea miti hadi akaanza kutembea wima.Mkuu wa kundi la utafiti
amesema kwamba ugunduzi huo unatoa ufahamu wa kwanza kuhusu mabadilio
muhimu ya binaadamu.
Proffessa Brian Villmoare kutoka chuo cha Nevada mjini Las Vegas amesema
kuwa ugunduzi huo unatoa uhusiano kati ya binadaamu anayefanana na nyani kwa
jina Lucy aliyeishi miaka millioni 3.2 ilioipita na ambaye aligunduliwa mwaka
1974 katika eneo hilo
Lucy aliyefanana na maumbile ya
binaadamu ana uwezo kuwa alibadilika na kuwa binaadamu wa kawaida?Lakini rekodi ya taya hiyo kati ya mda ambapo
Lucy na nduguze waliishi na kutokea kwa mtu aliyekuwa na maumbile ya nyani
aliyekuwa na ubongo mkubwa miaka millioni 2 iliopita imepishana kwa miaka
mingi.
Taya hiyo ya chini ya mdomo ilio na miaka
millioni 2.8 ilipatikana na mwanafunzi raia wa Ethiopia Chelachew Seyoun katika
eneo la utafiti la Ledi-Geraru,katika jimbo la Afar Amesemakwamba alishangazwa
alipokiona kifusi hicho.
''wakati nilipokipata kifusi hicho ,nilijua
kwamba kina umuhimu mkubwa kwa kuwa huu ndio wakati unaowakilishwa na mabaki ya
watu wa zamani mashariki mwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment