Vituo hivyo vilisita kupeperusha matangazo kupitia mfumo wa digitali kulalamikia hatua ya serikali kung’oa mitambo yao ya analojia.
Vituo vinavyodhaniwa kuwa na ushawishi mkubwa nchini Kenya zimetangaza kuwa zitarejea hewani kuanzia saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki, baada ya majuma matatu gizani.
Mwandishi wetu Ferdinand Omondi anaeleza kuwa Citizen TV, KTN, NTV vimekuwa wakilumbana vikali na serikali kuhusu kuhamia mfumo wa digitali, hadi wakaenda mahakamani kutafuta suluhu.
Hata hivyo mahakama iliamua kuwa vituo hivyo havikuwa na la kufanya ila kufwata maagizo ya mamlaka inayosimamia masafa na mawasiliano nchini Kenya kwani walikuwa na muda wa kutosha kuweka mikakati inayohitajika kuhamisha matangazo yao kutoka masafa ya analojia hadi yale ya kisasa ya dijitalia.
Stesheni hizo ziliomba muda zaidi kuagiza visanduku vya kunga'mua masafa ya digitali kwa wateja wao huku wakilalamika kuwa kampuni zilizopewa leseni kusambaza masafa yao yalikuwa yakitoza ada ya mwezi ilhali hawakuwa wakilipia huduma na matangazo kutoka kwa stesheni.
Sasa wanarejea katika miale ya digitali wakianzia Nairobi, na baadaye sehemu zingine za nchi.
Walipokuwa gizani, stesheni ya K24, inayomilikiwa na kampuni ya Media Max iliongeza idadi ya watazamaji kwa zaidi ya asilimia 170%
Huku haya yote yakijiri, BBC imearifiwa kuwa kituo cha serikali cha KBC kingali kinapeperusha vipindi vyake kwenye mtandao wa analogue sehemu za mashambani, ambako siku ya kuhamia masafa ya digitali ni tarehe 30 Mwezi Machi.
0 comments:
Post a Comment