Tuesday, May 19, 2015

   

Jumanne
 


UTUME WA YESU

 

Mithali ya Mwana Mpotevu: Sehemu ya 2
4. Kurudi nyumbani (Luka 15:17–20) kuliashiria safari ya toba. Safari ilianza “‘alipozingatia moyoni mwake.’”Utambuaji wa pale alipokuwa, na ulinganishajiwa jinsi nyumba ya babaye ilikuwa, ulisababisha msukumo wa “kuondoka” na “kwenda”
kwa babaye. Mwana mpotevu anarudi nyumbani akiwa na mazungumzo yenye sehemu nnezinazoelezea maana hasa ya toba ya kweli.
Kwanza, kuna utambuaji wa baba kama “‘baba yangu’” (aya 18). Sasa mwana mpotevu anahitaji kujitegemeza na kuutumaini upendo na msamaha wa babaye, kama vile sisi tuhitajikavyo kujifunza kuutumaini upendo na msamaha wa Baba yetu wa mbinguni.
Pili, Ungamo: kile mwana mpotevu alifanya hakikuwa ni kosa la kutofanya maamuzi mazuri, bali ilikuwa ni dhambi dhidi ya Mungu na babaye (aya 18).
Tatu, majuto: “‘sistahili’” (aya 19). Utambuaji wa kutostahili kwa mtu na ulinganishaji wa kutostahili huko na ustahili ule wa Mungu, ni muhimu sana kwa ajili ya toba ya kweli kufanyika.
Nne, ombi: “‘Nifanye’” (aya 19). Kujisalimisha kwa chochote kile ambacho Mungu anapenda ni mwisho wa toba. Mwana amerudi nyumbani.
5. Baba asubiriye (Luka 15:20, 21). Kusubiri na kukesha, huzuni na tumaini, vilianza wakati mwana mpotevu alipotoka nyumbani. Kusubiri huko kuliisha wakati baba alipomwona “‘Alipokuwa angali mbali,’” na kisha “‘akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana’” (aya 20). Hakuna mfano mzuri utupatiao picha halisi ya tabia ya Mungu kama huu wa baba asubiriye.
6. Jamii isherehekeayo (Luka 15:22–25). Baba alimkumbatia mwana, akamvika vazi jipya, akamvika pete kidoleni mwake na viatu miguuni pake, na akaamuru sherehe ifanywe. Jamii ikaanza kusherehekea.Ikiwa kuondoka nyumbani kuIikuwa ni kifo,
kurudi kulikuwa ni kufufuka, na huko kulistahili kusherehekea. Ni kweli kabisa kwamba mwana huyo alikuwa ni mpotevu, lakini bado alikuwa ni mwana, na kila mwana atubuye huwa analeta furaha mbinguni (aya 7).
7. Mwana mkubwa (Luka 15:25–32). Mwana mdogo alikuwa amepotea alipotoka nyumbani na kwenda nchi ya mbali; mwana mkubwa alikuwa amepotea kwa sababu, ijapokuwa alikuwa nyumbani kimwili, moyo wake ulikuwa nchi ya mbali. Moyo kama
huo huwa na hasira (aya 28), unalalamika, na hujiona kuwa una haki (aya 29), na hukataa kumtambua ndugu. Badala yake, humtambua tu “‘huyu mwana wako,’” aliyetumia vitu vyote (aya 30). Tabia ya mwana mkubwa kwa babaye ni sawa na ile ya Mafarisayo ambao walimshitaki Yesu na kusema: “‘Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao’” (aya 2). Neno la mwisho la baba kwa mawanawe mkubwa laakisi tabia ya mbingu kwa wadhambi wote watubuo: “‘“Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana”’” (aya 32).


        

Jiweke kwenye viatu vya mwana mkubwa. Hata kama mawazo yake yalikuwa ni mabaya, ni kwa nini inaonekana kama “alikuwa na haki” ya kuhisi jinsi hiyo? Ni kwa namna gani kisa hiki kinadhihirisha jinsi injili huenda zaidi ya kile ambacho twaweza kuona kama “ni haki” kingefanywa hivyo?
       
      

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA