Wednesday, May 20, 2015

   

Jumatano
 


UTUME WA YESU

 

Fursa Zilizopotea
Ijapokuwa Yesu alikuja kutafuta na kuokoa wale waliopotea dhambini, hamlazimishi yeyote kuukubali wokovu anaoutoa. Wokovu ni bure na unapatikana kwa wote, lakini mtu anapaswa aikubali zawadi hii itolewayo bure kwa imani, na ataweza kuishi maisha yanayoenda sawa na mapenzi ya Mungu. Muda tulionao kwa ajili ya uzoefu kama huo ni wakati tunaishi katika ulimwengu huu; hakuna nafasi nyingine kando na hii.
Soma Luka 16:19–31. Ujumbe wa msingi wa mithali hii ni upi?
Mithali hii imeandikwa katika Luka tu, na inafundisha kweli mbili kuu kuhusu wokovu: umuhimu wa “leo” katika mchakato wa wokovu na kutokuwepo kwa fursa ya wokovu baada ya kifo. Leo ndio siku ya wokovu.Mithali haifundishi kuwa kuna jambo lolote ovu kwa kuwa tajiriau uzuri wowote kwa kuwa maskini. Kile inafundisha ni kwamba fursa ya kuokolewa naya kuishi katika wokovu ipo wakati mtu yupo katika ulimwengu huu. Tajiri au maskini, mwenye elimu au asiye elimu, mwenye uwezo au asiye na uwezo, sote hatuna fursa ya pili. Wote wanaokolewa na kuhukumiwa kulingana na tabia zao za leo. “tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa” (2 Kor. 6:2).
Pia mithali inafundisha kwamba zawadi ya milele haihusu mali zozote zile tulizo. Mtu tajiri alikuwa akivaa “‘nguo za rangi ya zambarau na kitani sai, na kula sikuzote kwa anasa’” (Luka 16:19) lakini alikosa kitu muhimu katika maisha ambacho ni: Mungu. Mahali popote ambapo Mungu hatambuliwi, hata watu wengine pia hawatatambuliwa.Dhambi ya mtu tajiri haikuwa katika utajiri wake, bali ilikuwa ni katika kutotambua kuwa familia ya Mungu ni pana kuliko alivyoichukulia.
Hakuna fursa ya pili ya wokovu baada ya kifo. Ukweli wa pili ambao hauepukiki Yesu afundishao ni kuwa, hakuna nafasi ya pili ya wokovu baada ya kifo. “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Ebr. 9:27). Kidokezo kingine cha mithali hii ni kuonyesha watu kuwa, tumepewa ushuhuda mwingi mno katika maisha haya unaotusaidia kufanya uamuzi wa kuwa upande wa Mungu au kuwa kinyume Chake. Thiolojia yoyote ile ifundishayo juu ya kuwepo kwa aina yoyote ya “fursa ya pili” baada ya kifo ni ya uongo.

        

Huwa tunapenda kuzungumzia juu ya kiwango kile Mungu anatupenda na yote ambayo ametufanyia na yale ambayo anatufanyia ili kutuokoa. Mithali hii yapasa itufundishe nini kuhusu hatari ya kuuchukulia upendo na zawadi ya Mungu ya wokovu kama kitu rahisi?
       
      

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA