Thursday, May 21, 2015

   

Alhamisi
 


UTUME WA YESU

 

Nilikuwa Kipofu Lakini sasa Ninaona
Kauli ya kiutume (mission statement) ya Yesu kwamba alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea ni thibitisho la huduma ya ukamili (a holistic ministry). Alikuja kuwafanya waume kwa wake wawe kamili (whole), kuwabadilisha kimwili, kiakili,
kiroho, na kijamii. Luka anatupatia mambo mawili yanayoonyesha jinsi Yesu alivyorejesha watu wawili waliokuwa wamevunjika moyo na kuwafanya kuwa kamili. Mmoja alikuwa ni kipofu kimwili, wa pili alikuwa natatizo la kiroho; wote
wawili walikuwa wametengwa kijamii—mmoja alikuwa ni mwombaji na mwingine alikuwa ni mtoza ushuru. Lakini wote wawili walihitaji utume uokoao wa Kristo na hakuna hata mmoja kati ya hao ambaye hakuwa moyoni mwake au ambaye
hakuweza kumikia.
Soma Luka 18:35–43. Hii inatufunza nini kuhusu namna tupaswavyo kumtegemea Mungu? Ni nani miongoni mwetu ambaye hajawahi kulia na kusema, “Nirehemu”?

Marko anamtaja mtu huyo kama Batimayo (Marko 10:46). Alikuwa ni muombaji nje ya mji wa Yeriko. Akiwa na changamoto ya kimwili, kijamii na akiwa amekumbwa na ufukara, kwa ghala akajikuta katika muujiza wa mbingu: “Yesu wa Nazareti anapita” (Luka 18:37), na imani yake ikamuongoza kulia na kusema, “‘Ee Mwana wa Daudi, unirehemu!’” (aya 39). Imani haihitaji macho au masikio, miguu au mikono, bali huhitaji moyo ambao unaunganika na Muumba wa ulimwengu.
Soma Luka 19:1–10.Ni nani ambaye alikuwa ni“kipofu” katika kisa hiki?
Ni Luka tu ndiye anaandika kisa cha Zakayo, ambacho ni cha mwisho kati ya visa vingi ambavyo Yesu alikutana na watu waliokuwa wamekataliwa kijamii. Utume wa Kristo, wa kutafuta na kuokoa kile kilichopotea, ulikamilika wakati alipokutana na
Zakayo. Zakayo alikuwa ni mtoza ushuru mkuu wa Yeriko, na ambaye alikuwa ni mdhambi mkuu machoni pa Mafarisayo waliokuwa katika mji huo, lakini alikuwa ni mdhambi mkuu aliyetafutwa na kuokolewa na Mwokozi. Yesu alitumia sehemu
na njia zisizo za kawaida ili kukamilisha utume Wake. Mkuyu, mtu mwenye shauku aliyetaka kujua Yesu alikuwa ni nani, na Bwana mwenye upendo anayeagiza watu waweze kushuka chini, kwani alikuwa na mlo wa mchana aliouomba Yeye mwenyewe
uliokuwa umeandaliwa kwa ajili Yake. Lakini muhimu zaidi ni kuwa Yesu alikuwa na kitu cha kusema: “‘Leo wokovu umeika nyumbani humu’” (Luka 19:9) na alisema baada ya Zakayo kutengeneza mambo na kuwa sawa (aya 8).


        

Ni rahisi kuona makosa na upungufu wa watu wengine, si ndio? Lakini mara nyingi twaweza kuwa vipofu kwa makosa yetu wenyewe. Ni sehemu gani za maisha yako ambazo wahitaji kuzifanyia matengenezo, kuungama, na kupata ushindi dhidi ya kitu ambacho umejaribu kukiacha kwa muda mrefu?        
       
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA