Friday, May 22, 2015

   

Ijumaa


UTUME WA YESU

Jifunze Zaidi: “Kwa kutumia mfano wa kondoo aliyepotea, Kristo hakuangazia mtu mdhambi binafsi tu, bali pia dunia hii moja ambayo imeasi na imeharibiwa na dhambi.”—Ellen G. White, Christ’s Object Lessons, p. 190.
Kwa thamani ya nafsi moja: “Ni nani awezaye kuitathmini thamani ya nafsi moja? Je wataka kuijua thamani yake, nenda Gethsemane, na hapo, mtazame Kristo akipitia kipindi cha masaa ya uchungu, wakati jasho lilikuwa kama matone ya damu. Mtazame Mwokozi akiinuliwa msalabani. . . .ukikumbuka kuwa, hata kwa ajili ya nafsi moja, Kristo angeweza kuutoa uhai Wake, sasa waweza kadiria thamani ya nafsi moja.”—Page 196.
Maswali ya Kujadili:
1. Wakati dini zote zinaangazia mwanadamu akimtafuta Mungu, Ukristo unamuangazia Mungu akiwa ndiye mtafutaji: Adamu, uko wapi (Mwa. 3:9)? Kaini, yuko wapi nduguyo (Mwa. 4:9)? Eliya, unafanya nini hapa (1 Fal. 19:9)? Zakayo, shuka chini (Luka 19:5). Umekuwa na uzoefu gani wa namna Mungu
amekutafuta wewe?
2. Hebu tazama tena swali la mwisho la fundisho la siku ya Alhamisi. Ni kosa gani kubwa ambalo mwana mkubwa alifanya? Ni kasoro gani za kiroho zilidhihirika katika tabia yake? Kwa nini ni rahisi kwetu kuwa na kasoro kama
hiyo kwa urahisi kuliko tudhanivyo? Tazama pia Mathayo 20:1–16.
3. Katika kisa cha mtu tajiri na Lazaro, Yesu alisema kwamba, hata kama mtu angekuja toka kwa wafu, wapo wale ambao hawangeamini. Ni kwa njia gani mithali hii ilielezea mjibizo (reaction) wa baadhi ya watu kuhusiana na ufufuo wa Yesu, ambao baadhi yao bado hawakuamini hata ijapokuwa upo ushahidi wenye nguvu wa ufufuo Wake?
4. Moja wapo ya jambo la kupendeza kuhusu huduma ya Yesu ya uokozini usawa ambao kwa huo aliwachukulia watu wote, kama vile yule kipofu mwombaji na Zakayo au Nikodemo na mwanamke Msamaria. Msalaba unaonyesha usawa wa watu wote mbele za Mungu. Ukweli huu muhimu unatusaidiaje katika swala la namna tunavyopaswa kuwachukulia wengine, hata wale ambao—kwa sababu ya siasa, utamaduni, ukabila—tumekuwa tukiwachukulia vibaya? Kwa nini tabia hiyo ni kinyume kabisa na Yesu?
5. Linganisha kisa cha mwana mpotevu na kile cha tajiri na Lazaro. Ni kwa namna gani visa hivi viwili vinawekeana usawa
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA