Monday, June 22, 2015

Nderemo na vifijo vilikuwa katika kanisa la Waadventista Wasabato Ilala jijini Dar es Salaam Jumapili hii ambapo aliyekuwa muimbaji wa Sauti ya kwanza katika kikundi cha Triumph Generation maarufu kama Wana TG wa kanisa la Wasabato Mbezi Luis jijini, Irene Nicco Urio, 22 maarufu kwa jina la Irene Kiangi alipounganishwa kwa ndoa takatifu na Bw. Willy Mzungu dugilo, 42.
Ndoa ya wawili hawa ilifungwa na Mchungaji Charles Mjema na baadae kuelekea katika sherehe katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Sinza Makaburini.
Injilileo Blog ilikuwa moja wa Shuhuda katika ndoa hii na hapa tunakuletea angalau matukio machache ya picha...
Bwana Harusi, akienda kwa mwendo wa taratibu kumpokea Bibi Harusi
Bibi Harusi Akisogea kumulaki Bwana harusi
Kwaya ya kanisa la Waadventista Wasabato Kigogo ambapo Bwana Harusi anasali
 Injilileo Timu, tunawatakia maisha mema yenye baraka tele, Aminaa!

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: , ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA