Sunday, June 14, 2015

Hatimaye mpambano mkali juu ya uovu na wema kati ya MUNGU wa Mbinguni na shetani umekamilika katika mji wa Tunduru mkoani Ruvuma ambapo watumishi wa Mungu muinjilisti Eliud Enock kutoka mtaa wa Mzizima jijini Dar es Salaam wakishirikiana na Ustaadhi Suleiman Moshi kwa muda wa majuma matatu waliwadhihirishia watu ni kwanamna gani Shetani alishindwa tangu zamani na hivyo wanapaswa kumchagua Mungu.
Kupitia mikutano hiyo iliyokuwa inafanyika katika viwanja vya Ujenzi wilayani Tunduru na kuhudumiwa na waimbaji wa Heaven Traveller's Generation kutoka katika kanisa la Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, Shetani alihaibishwa pale watu 14 walipomkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao kwa njia ya ubatizo, Uliofanywa na Mch. Mwashinga Jr kutoka Songea.
Jina la Bwana lipewe sifa kwa ushindi ulioonekana kwani kupitia mikutano hiyo, watu wote wageni kwa wenyeji walimuona Mungu upya na hii inafuatia mahojiano na shuhuda ambazo Injileo blog ilifanya na baadhi ya watu waliokiri kwamba mikutano hii ilikwenda mjini hapo kwa wakati muafaka.
Tunakusihi unapokuwa katika maombi yako, likumbuke jeshi hili jipya.
Na haya ni baadhi ya matukio katika picha yaliyotokea siku ya UBATIZO...
Waliokuwa Wahubiri katika Mikutano hiyo, Kushoto ni Ustaadhi Moshi na muinjilisti Eliud
Kikundi cha Heaven Traveller's Generation wakiimba kufungua huduma
Kikundi cha Heaven Traveller's Generation wakiimba kufungua huduma
Mch. Mwashinga Jr akitoa somo kabla ya viapo
Mch. Mzava akiendesha huduma ya viapo
Hatimaye safari ilianza
Kuelekea Yordan
Kuelekea Yordan
Kuelekea Yordan
Shemasi wa Kanisa Bwana Msigwa akimalizia maandalizi ya mto wa kubatizia
Ombi la kufungua huduma
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA