Sunday, June 14, 2015

Mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Democratic bi Hillary Clinton, tayari amejitokeza kwa mara ya kwanza kwa umma wa watu wa New York tangu alipotangaza nia yake ya kuwania kiti cha uraisi nchini Marekani kinachoshikiliwa na rais mweusi Barrack Obama.
Bi. Clinton akisisitiza jambo
Bi. Clinton,67 mwenye sera pekee ya kutetea maslai ya chini ya Wamerakani, kuhakikisha kila mtu anfikia ndoto yake aliyo nayo, alisindikizwa na mumewe aliyewahi kushikiria kiti hicho Bw. Clinton pamoja na binti yao Chelsea, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanatoa takwimu ya kwamba ushawishi wake kwa wananchi unaendea kushuka siku hadi siku tangu alipojitokeza kwa maelfu wa mashabiki wake kutangaza nia yake ya kuwania kiti hicho. 
Mama, Mtoto na Baba

Kwa ufupi haya ni baadhi ya maneno ambayo Bibi huyu aliwahi kunukuliwa akisema katika kutilia mkazo sera yake:
"Kila mmoja wetu anahaki ya kupata maisha mazuri tu na kuishi kwa amani na ustawi kadri ya uwezo wake aliopewa na mwezi mungu''
''Hiyo ndiyo ndoto yangu hiyo ndiyo vita tunayopaswa kupigania ''alisema bi Clinton.
''Babangu mimi alikuwa mtoto wa mfanyikazi wa kawaida kiwandani aliyejikakamua na kuanzisha biashara ndogo''
"Mamangu pia japo hakuenda chuoni alinisomesha nikahitimu chuoni''
''Kila Mmoja wetu anahitaji kuwa na ndoto na mtu anayemuiga ambaye ameanzia chini maisha yake na kuimarika kufikia ufanisi wa kutajika".
Watu walioshindwa kuficha hisia zao
 Picha na bbcswahili.com
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA