Thursday, June 18, 2015

Kituo cha runinga ya Morning Star kupitia kipindi chake cha Ongeza Maarifa, kinakuletea kwa ukaribu mambo mengi na ujuzi ulio katika jamii ambao kwa namna moja au nyingine usingeweza kukutana nayo. Wiki hii inakukutanisha na kijana Ismail Abdallah John kutoka katika kanisa la Waadventista Yombo Dovya, mtaalam wa Usanifu majengo ambaye kwa uwezo mkubwa anaweza akaandaa ramani na kuiweka katika muonekano wa umbo kama jengo halisi.
Bw. Ismail Abdallah John, Ndani ya Studio za Morning Star
Je, unatamani kuweza kufanya kazi hii? Je, unatamani kufahamu inatumia muda gani kumaliza kazi hii? Je, anatatumia vifaa na kiasi gani? Je, unatamani kujenga na je, anaweza kukusaidia kuepuka majanga ya mafuriko? 
Mfano wa Umbo la jengo la Kanisa la Waadventista wasabato Yombo Dovya jijini Dar es Salaam
Usihofu, majibu ni haya...
"Mtangazaji wako Mazara Edward Matucha atakusaidia kukata kiu ya kile ambacho unatamani kufahamu kutoka kwa wataalamu wa aina hii kwani amezungumza naye mambo mengi ambayo ni mahitaji ya kila siku".
Mazara Edward Matucha, Mtangazaji wa kipindi cha Ongeza Maarifa
Timu ya INJILILEO BLOG tunatoa pongezi za dhati kwa kijana huyu lakini zaidi kwa waandaaji wa kipindi hiki kwa kutoa fursa za kuwasogeza karibu vijana kama hawa. Tuna ahidi kuwa karibu na kipindi hiki kwa kukuendelea kukupa taarifa zihusuzo kipindi hiki kwa ujumla.
Mungu na awabariki Nyote, Amina!!

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA