Monday, June 29, 2015


June 25, 2015 | Silver Spring, Maryland, United States | Mylon Medley/ANN
Mkutano Mkuu (ufanyikao kila baada ya miaka miatano) ndiyo mkutano mkuu kuliko mingine yote ya Kanisa la Waadventista wa Sabato. Katika kipindi cha siku kumi za mkutano huo, viongozi wa kanisa huchaguliwa na shughuli mbalimbali za kuliongoza kanisa jinsi ya kutekeleza utume wake hufanyika.
Inapokuja swala la kuwawezesha maafisa wa kanisa, zaidi ya wajumbe 2,000 huwa na jukumu la kupigia kura mapendekezo yatokanayo na vikao vya Kamati Kuu vilivyopita, kikao kingine cha pili kwa hadhi katika kuliongoza kanisa. 
Hata hivyo, ujapo wakati wa kuwachagua viongozi wa Kanisa, wakiwamo Wenyeviti wa makao makuu ya kanisa, viongozi wa divisheni na viongozi wa huduma mbalimbali za kanisa, wajumbe 252 huteuliwa kuunda kibaraza cha uchaguzi. Lakini ni nani hawa wanaounda kibaraza cha uchaguzi? Wanachaguliwaje? Na nini hasa jukumu lao?
KUUNDA KAMATI
Wajumbe 252 wa kibaraza (kamati) cha uchaguzi hutokana na wajumbe 233 kutoka divisheni 13 za kanisa, na wajumbe 19 kutoka makao makuu ya kanisa, ijulikanayo pia kama General Conference. 
Kwa kuwa uchaguzi huanza kwa mchakato wa kuchagua wajumbe wa kibaraza, kibaraza cha uchaguzi (kwa mujibu wa Myron Iseminger – aliye msaidizi wa Katibu Mkuu wa General Conference) huundwa siku ya kwanza ya mkutano wa General Conference. kila divisheni huruhusiwa kutuma asilimia kumi ya ya wajumbe wake kwenye kibaraza cha uchaguzi. Kwa upande mwingine, General Conference huruhusiwa kutuma asilimia nane ya wajumbe wake.
Kuna mambo mengine yanayohitaji kuzingatiwa linapokuja swala la kuchagua wawakilishi wa kibaraza cha uchaguzi. Kwa mfano, kila anayechaguliwa ni lazima awe mjumbe anayestahili kupiga kura kwenye Mkutano Mkuu wa Sesheni.
Pia, wajumbe wanaochaguliwa kuingia kwenye kibaraza cha uchaguzi hawawezi kuchaguliwa kuwa maafisa wa General Conference. Maafisa hao ni Wenyeviti wa General Conference na Divisheni zake, Makamu wenyeviti wote, makatibu, makatibu wasaidizi, makatibu wenza, Wahazini wasaidizi, Wahazini wenza, Maofisa wa Divisheni, Maafisa wa Huduma ya Ukaguzi ya General Conference, na viongozi wa idara za General Conference.
Kwa maneno mengine, ikiwa mjumbe anatumika kwa nafasi inayochaguliwa kwenye sesheni hawezi kuwa mjumbe wa kamati ya uchaguzi. 
Unaweza kuuliza, “Ni nani sasa amebaki ili awe mjumbe wa kibaraza cha uchaguzi?” kibaraza cha uchaguzi kimesheheni wenyeviti na maofisa wa Union, viongozi wa konferensi, washiriki wa kawaida, viongozi wakuu wa taasisi za General Conference, zikiwemo shule, hospitali, na taasisi ya Ellen G. White. 
WAHUSIKA WAKUU KWENYE KAMATI YA UCHAGUZI
Mara tu idadi ya wajumbe 252 inayounda kamati ya uchaguzi inapokuwa imekamilika, kamati hupelekwa kwenye chumba cha faragha ambako huanza mara moja kutekeleza majukumu yake, wakianzia na kumchagua mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, makamu mwenyekiti, katibu, na katibu mwenza. Baada ya maafisa hao kujulishwa majukumu yao, kamati chini ya uongozi wa mwenyekiti huanza mchakato wa kuchagua viongozi wa ngazi za juu za kanisa. 
Bob Kyte, Mwenyekiti wa Adventist Risk Management, aliyetumika kama mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa sesheni ya General Conference ya mwaka 2010, anasema jambo moja la kuzingatia kwenye chumba cha uchaguzi ni kutofautiana siyo katika lugha tu, bali hata mitazamo ya njia ipi ni bora kamati yaweza kuifuata katika mchakato wa kuchagua majina. “Moja ya changamoto kubwa ilikuwa kujaribu kuchanganya mazoea ya namna wanavyoendesha vikao vya uchaguzi kama kanisa kote ulimwenguni.” Alisema Kyte.
Wakati Kiingereza ndiyo lugha rasmi ya mikutano yote ya mashauri ya kanisa, bado wafasiri huwepo wakati wote wa mikutano ya kamati kuhakikisha taartifa inawafikia kwa ufanisi wajumbe wa kamati wazungumzao lugha zingine. 
Wahusika wengine wawili wa kamati ni mameneja wa mfumo wa kielektroniki, ambao kupitia kwa mashine wanazozisimamia kura zote za mkutano hupigwa. Mameneja hao huhifadhi kila jina lililopendekezwa na majina yote yaliyochaguliwa kwa kila nafasi. Kumbukumbu zao huwekwa kwenye ofisi ya kanisa ya utafiti, takwimu, na uhifadhi wa nyaraka.
MCHAKATO WA UTEUZI
Wakati wa kuanza kila siku, mmoja wa maafisa hutupatia somo la Maandiko. Viongozi pia hualika uwepo wa Mungu ili kuongoza katika mchakato wa kufanya maamuzi. “Tuliomba kabla ya kila kura ili Mungu atuongoze katika kuchagua,” alisema Kyte. Nafasi ya kwanza kamati ya uchaguzi inayofikiria ni mwenyekiti wa General Conference. Mara mwenyekiti anapochaguliwa hutumika kama mshauri kwa kamati ya uchaguzi kwa mchakato mwingine wote uliobaki. 
Baada ya mwenyekiti kuchaguliwa, kamati huchagua majina ya Katibu Mkuu na Mhazini wa General Conference. baada ya maafisa wa General Conference kuchaguliwa, kamati huchagua majina ya nafasi zingine zilizobakia zitakazojazwa wakati wa sesheni.
Mara kamati inapochagua jina, afisa wa kamati, au afisa aliyeteuliwa kutoka General Conference, humjulisha mhusika kuhusu msapendekezo ya kamati. Afisa pia humjulisha aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo juu ya mabadiliko hayo kabla ya kumjulisha yule aliyependekezwa kuchukua nafasi yake.
“Nyakati fulani, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, maafisa wa kamati ya uchaguzi, wangeweza kufanya zaidi ya kuwajulisha walioteuliwa. Katika nyakati fulani tuliwatia moyo waliochaguliwa kupokea nafasi hizo.” Alisema Cindy Tutsch, mkurugenzi mwenza mstaafu wa taasisi ya Ellen G. White, aliyetumikia kamati kama katibu wakati wa sesheni ya General Conference ya mwaka 2010, na ambaye baadaye alishika nafasi ya makamu mwenyekiti wa kamati, baada ya aliyeshika nafasi hiyo kuchaguliwa kama makamu mwenyekiti wa General Conference.
Mara baada ya aliyependekezwa kujulishwa, maafisa wa wa kamati ya uchaguzi huelekea ukumbini ambako mashauri hufanyika. Mwenyekiti wa kamati ya mipango aliyekuwa zamu hukatiza kilichokuwa kinajadiliwa, ili kusikiliza mapendekezo ya kamati, au taarifa ya kamati ya uchaguzi. Nyakati fulani taarifa huhusisha mapendekezo ya makundi mbalimbali. Ingawa taarifa ya kamati ya uchaguzi huchukuliwa kama mapendekezo, ni mara chache kwa wajumbe wa session kukataa taarifa hiyo ya kamati. 
Ikiwa mjumbe yeyote atakuwa na udhuru juu ya taarifa hiyo, ataombwa aseme udhuru wake baada ya taarifa yote kusomwa, na hapo mjumbe ataalikwa kama mgeni kwenye kamati ya uchaguzi kueleza sababu zake. Baada ya kutoa sababu zake mjumbe ataruhusiwa kuondoka ili kupisha kamati kufanya maamuzi kama jina libaki ama liondolewe.
‘UTENDAJIKAZI WA KANISA’
Ingawa kundi la kamati ya uchaguzi ni dogo ukilinganisha na waumini wa kanisa la kiulimwengu wanaofikia milioni 18.4, kazi ya kamati ya uchaguzi ni ya muhimu sana kwa utendaji kazi wa kanisa la Waadventista wa Sabato. ni muhimu kwa kikundi cha wajumbe 252 walioteuliwa kutumika kutenda kazi kwa karibu na Roho Mtakatifu, na kunyenyekezwa naye ili kujaza nafasi zote zinazohitajiwa na session.
Na Mchungaji Stephen Letta                                                                                

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA