Wednesday, June 17, 2015

👉1Timotheo 4:12 "Mtu awaye yote asiudharau UJANA wako, bali uwe KIELELEZO kwao waaminio, katika USEMI na MWENENDO, na katika UPENDO na IMANI na USAFI".
👉Kama kuna TATIZO SUGU kwa vijana wa leo, ni kuwa na UPENDO FEKI ambao huishia Uchumba kuvunjika au Mahusiano yenye kuleta huzuni. Ni jambo la kawaida kusikia 'Ahhh yule DEMU! nilisha MBWAGA siku nyingi niko na chombo kingine'. Vijana wa KIKE na wa KIUME, wanaingia kwenye mahusiano ya kubahatisha na kulazimika kuwa na 'SPARE TYRE'.
👉Neno USIZINI, limekuwa msamiati wa wazee wa kale, na vijana wengine wanasaka Kuchumbia binti ambaye hajaliwa na Mende (BIKIRA), wakati yeye mwenyewe sio safi. Kupima (KU TEST) kabla hata ya kuanzisha rasmi uchumba, ndio dili kwa vijana wengi wa kizazi hiki cha UOVU, matokeo yake ni Vilio na Huzuni kwa wanaobwagwa. Pia kuna Mabinti wenye tamaa, nakuwa mchumba mwaminifu, huku ana buzi (PEDESHEE) linalompatia mahitaji, utakuta zee zima linaitwa Baby.
👉 NENO LA LEO, Mungu bado anawahitaji vijana kuwa WAAMINFU, na kuwa kielelezo, UPENDO wa kweli ni ule unaojegwa na Mungu, unakuwa na HOFU ya Mungu. Ukiona Kijana anadai anakupeda na huku anakimbilia Ngono, huyo sio mcha Mungu na Mahusiano mtakayoanzisha yatakuwa chini ya Utawala wa Ibilisi, na mwisho wake ni MAJUTO NA KUDHARAULIWA, utaishia kuonjwa kama mboga na mwisho Kuchacha.
👉Na Mabinti msitoe Mimba, laana yake ni kubwa, mtakuja kutafuta watoto msimpate. Hebu leo kila mmoja aamue kupatana na Mungu kwa usema UKWELI, kama huna mpango wa kumuoa au kuolewa na huyo uliyemtolea ahadi, MWAMBIE, kumpotezea muda ni Dhambi itakayokugharimu.
👉WITO: Wema wa Mungu bado upo, haijalishi maisha uliyopitia siku za nyuma, amua kumrudia Mungu, achana na ZINAA, acha udanganyifu na UTAPELI wa mapenzi. Mungu ni mwaminifu atakupatia MWENZI wa maisha. Amini tu, kwake yote yanawezekana, atafanya njia pasipo njia. Leo mwambie shetani BYE BYEE! Narudi nyumbani kwa Baba. 👉NAOMBA VIJANA WOTE WAPATE SOMO ILI👈
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE AMANI, FURAHA NA BARAKA.
Na. Ev. Eliezer Mwangosi - Tel. 0767210299, Em. eliezer.mwangosi@yahoo.com.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA