Thursday, July 09, 2015

Maisha ya Mwanadamu katika ulimwengu huu ni mafupi sana.

Isaya 58:1 Piga kelele usiache, paza sauti yako kama tarumbeta; uwahubiri watu wangu kosa lao, na yumba ya Yakobo dhambi zao

Je Ni kweli Yesu atakuja? Ndiyo.

Katika Biblia kuna zaidi ya mafungu 1500 yanayoelezea tukio la kurudi kwa Yesu mara ya pili.

Yohana 14:1-3  Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi nanyi muwepo.

Atakuja kwa jinsi gani?
Mafungu zaidi ya 40 yanaelezea jinsi Yesu atakavyokuja, hebu tuangalie mafungu yafuatayo:

Ufunuo 1:7  Tazama yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake.

Mathayo 24:26-27, 29-31 Basi wakiwaambia, yuko jangwani, msitoke, yumo nyumbani, msisadiki, kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 29. Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, nanyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni, ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamuona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.

Soma pia Mathayo 16:27 na  Mathayo 25:31-33 – Atakuja kwa utukufu mwingi – Ndipo atakapobagua wanadamu katika makundi mawili – KONDOO NA MBUZI. Walio mkono kuume watapewa kuurithi uflme waliowekewa na Baba tangu kuumbwa ulimwengu.

Je ndugu zetu waliokufa itakuwaje?

1Wathesalonike 4:13, 16-17 Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini 16.

Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa Kwanza. 17. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani. Soma pia 1Korintho 15:50-56.

Ufunuo 20:13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, wakahukumiwa kila mtu kwa kadri ya matendo yake.

Je kuna mtu anayejua siku ya kuja Yesu Kristo?

Mathayo 24:36  Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.

NB: Luka 17:34-36 Nawambia, usiku huo watu wawili watakuwa ktk kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa mmoja ataachwa n.k. Pia soma Mathayo

24:40-41. Shetani ameyatumia mafungu haya kueneza Somo la Unyakuo wa Kanisa kwa siri, kabla ya kuja kwa Yesu Kristo katika Utukufu na wote wakimuona.

HATARI ILIYO MBELE YETU JUU YA SOMO HILI LA UNYAKUO WA SIRI

Kutwaa haina maana unyakuo wa Siri bila wengine kuona, ina maana ya kutenga:

Mfano, ‘Mathayo 17:1 – Yesu akamtwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani’, hii haina maana walinyakuliwa kwa siri bila wengine kuwaona.

UTAWALA WA MIAKA SABA BAADA YA UNYAKUO WA KANISA SIO FUNDISHO LA BIBLIA

Athari ya Fundisho hili:

1. Fundisho hili ni la Roho za kuzimu zinazowafanya watu waendelee na dhambi wakisubiri kuja kutubu katika kipindi hiki cha miaka saba.

2. Linawaongoza wakristo wengi kutojishughulisha kujifunza juu unabii wa siku za mwisho hasa juu ya Mpinga Kristo na Ibada ya Jua – Roho wa nabii wa Uongo ndiye inayefanya kazi kwa ishara na Miujiza kuwaongoza wengi wawe mateka ya Adui na kumpa nguvu mpinga Kristo katika pambano kati ya Mungu wa Kweli na Shetani aliyesimamisha Ibada ya Jua kama alama yake.

AMRI YA JUMAPILI (SUNDAY LAW) itakapotangazwa bila kunyakuliwa watajikuta wamechelewa.

NB: Yesu akija mara ya pili waovu watakufa wote, na watakatifu watakuwa mbinguni hadi miaka 1000 ipite ndipo waovu wote pamoja na shetani watatupwa katika ziwa la Moto. Watakatifu watakaa milele katika mji mtakatifu Yerusalem mpya waliyoandaliwa. Soma Ufunuo 20:1 -15, 21:1-8.

WAKATI ULIOKUBALIKA KUSIMAMA UPANDE WA BWANA NI LEO UNAPOISIKIA SAUTI YA MUNGU


Na Mwinjilist: Eliezer Y. Mwangosi
Mobile Phone: 0767 210 299 
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA