Katika wakati huu ambapo dunia imetawaliwa na mambo mengi maovu yanayosababishwa na mmomonyoko wa maadili katika jamii.
- Je, elimu uliyopata imekuwezesha kulinda maadili katika jamii?
- Je, mazingira ya shule uliyosoma yamekupa msaada kiasi gani kufikia kiwango cha juu cha maadili?
- Je, unaiandaaje familia na jamii yako kwa ujumla kupata nafasi njema ya kunufaika zaidi au sawa na wewe katika nyanja ya maadili?
Majibu yote ya maswali hayo ni mepesi sana kupatikana kutoka kwa mwanafunzi aliyesoma au anayesoma katika shule ya msingi ya Kongowe.
Ni shule inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wasabato, inapatikana Kongowe, Kibaha katika mkoa wa Pwani. Inayo madarasa ya awali hadi darasa la saba.
Pamoja na masomo ya kawaida, inafundisha uchaji Mungu, Kujitegemea, Ukakamavu na mengine mengi ambayo yamekuwa ni changamoto katika maadili ya vijana katika jamii.
Hapa tunakuletea matukio katika picha ya baadhi ya wanafunzi wa shule hii, walipotembelea na kuabudu katika kanisa la Waadventisa Wasabato Ilala jijini Dar es Salaam.
 |
Kusanyiko katika Ibada ya pamoja katika Kanisa la Ilala |
 |
Baada ya Ibada ya asubuhi, walifanya shughuli ya upimaji afya bure wa Waumini, Pichani ni mmoja ya Wazee wa kanisa akipimwa afya |
 |
Mchana walionesha matendo ya ukakamavu na mambo mengine wanayojifunza |
 |
Mchungaji wa Vijana hao Emmanuel Rajabu kushoto akihubiri huku akisaidiwa katika kutafsiri kwa lugha ya kiingereza na mkuu wa shule hiyo |
 |
Mchana walionesha matendo ya ukakamavu na mambo mengine wanayojifunza |
|
 |
Mchana walionesha matendo ya ukakamavu na mambo mengine wanayojifunza |
|
 |
Mch. Emmanuel Rajabu akisalimiana na watu baada ya ibada |
 |
Vijana wadogo, wakisimamia zoezi la upimaji afya |
 |
Baadhi ya washiriki wakiwa katika foleni ya kusubiri huduma ya upimaji afya |
 |
Waliohudhuria katika ibada ya siku hiyo |
 |
Zoezi la upimaji likiendelea, hapo watu wakipima uzito na urefu na zoezi zima likisimamiwa kwa ustadi na vijana wadogo |
 |
Katika ibada ya siku hiyo |
 |
Moja ya wanafunzi katika shule za awali, akiwa katika tabasamu zito |
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Good school
ReplyDelete