Mathayo 5:44-45 "Lakini mimi nawaambia, wapendeni ADUI zenu,
waombeeni WANAOWAUDHI; ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye
mbinguni....."
Nilipokuwa nafuatilia post za wapendwa wengi na wakati mwingine kusikiliza wakiongea juu ya matokeo ya uchaguzi hasa wa Uraisi, nimesikitika kugundua kwamba wapendwa wengi wameghafilika na kutanga mbali na misingi ya wokovu wetu. Wengi wameruhusu shina la uchungu lichipuke ndani ya mioyo yao na hatimaye kuwatia unajisi (Soma Waebrania 12:14-15), roho za visasi na uadui zimetawala kuwasumbua wengi.
Katika somo langu la 30.08.2015, nilitoa somo lililosema: WATU WA MUNGU NA SIASA / UCHAGUZI, likitoa mwanga jinsi Mungu anavyohusika na tawala za jamii, na watu wa Mungu wanachopaswa kukifanya na namna ya kuyapokea matokeo. Baada ya matokeo nimegundua watu wa Mungu wengi hawajui jinsi Mungu anavyotenda kazi hasa katika michakato ya kupata watawala wa serikali inayojumuisha WAOVU NA WEMA, mawazo ya Mungu yako tofauti sana na mawazo yetu. Hivyo tunapoona mambo hayako sawa, tunapaswa kutulia na kutafuta hekima yake.
Neno linasema "Mpende Adui na Kumuombea", Jihoji Kama Mcha Mungu, baada ya matokeo ya uchaguzi na Raisi kuapishwa, iwe ni kwa haki au laa, umechukuwa hatua gani? Siku moja kabla ya Raisi kuapishwa nilisikia malalamiko mengi tena yenye uchungu na wengine kufikia kuombea Mabalaa yatokee ili asiapishwe. Hadi leo hii kuna wapendwa wengi wanaombea mabaya yatokee kwa Raisi aliye madarakani, ikiwa ni adhabu kutoka kwa Mungu. Kumbukeni Chama au Serikali haina Dini, ila ndani yake kuna wacha Mungu na Waovu. Kumbukeni Taifa la Israeli lilipigwa na kuhujumiwa haki na mataifa maovu kwa sababu tu ya maovu ya watu wachache.
KWA WATANZANIA: Wale wanaoamini kuwa wameporwa haki yao Kupitia mchakato wa uchaguzi, ni wakati wa kukaa na Mungu ili awape hekima ya kufanya maamuzi sahihi bila kutenda UOVU, wajichunguze na kujihoji, wakiona kuna uovu ndani yao juu ya jamii watubu na kuungama, ili Mungu ajidhihirishe juu yao kwa wakati. Waombeeni walioko madarakani kwa wakati huu, ili Mungu awape hekima na ufahamu wa kutenda mambo kwa HAKI. Kusudi la Mungu ni KUOKOA sio kupoteza roho, ombea waokolewe, wawe na hofu ya Mungu, ndipo mtapandishwa juu ya Vilima kwa wakati uliokubalika.
KWA WATANZANIA: Wanaoamini wameshinda kwenye uchaguzi; kwa hakika Mungu ndiye anayejua, kama ni kwa uhalali au laa. Kama nilivyotangulia kusema, ndani ya vyama na serikali kuna WAOVU na WEMA. Ikitokea Mungu ameruhusu mafanikio kwa njia isiyo halali, sio kwamba anakubaliana na uovu, ila kuna neema inamtafuta mmoja atubu, ili aokolewe. Huu ni wakati wa mpito wa kupimwa tena katika mizania ya Mungu. Kama kuna Uovu wowote ni wakati wa Kutubu ili Mungu awafanikishe katika HAKI. Kumbukeni hakuna AMANI Kwa Waovu (Isaya 48:22).
Kama ushindi ulikuwa ni wa halali, bado mnatakiwa kunyenyekea chini ya Mkono wa Mungu, ili azidi kuwakweza na kuwafikisha katika vilele. Bila Mungu hekima ya Mwanadamu ni patupu, shetani atawashinda na kuwa na hali mbaya kuliko matazamio ya watanzania. 1Petro 5:6-7.
HITIMISHO: Bwana Mungu anasema "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA" Isaya 55:8. Watu wa Mungu tunahitaji kuwa makini na kuomba hekima kwa Mungu, hasa tunapojihusisha na mambo ya Vyama vya siasa ambavyo havina misingi ya Dini. Sisi tunatazama kwa macho ili kutimiza makusudi na mapenzi ya mioyo yetu, lakini Mungu hayuko hivyo. Usishindwe na Ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema 'Warumi 12:21'.
Watu wa Mungu tunaoishi katika kazazi hiki kiovu, tunapaswa kuwa chachu ya kuleta AMANI, tukiwaombea waovu waokolewe, kuchukia UOVU sio kulipa visasi na kuombea mabaya, hizo ni roho za yule adui. Waovu wanaonywa kwa upendo, wanashauriwa, wanaombewa, wakiendelea na uovu unaotudhuru tutatumia vyombo vya sheria na kutafuta haki. Ni agizo la Mungu kuzitii Mamlaka zozote zilizowekwa katika Jamii - Warumi 13:1-7. Mwenye Mamlaka ya mwisho juu ya Kuziweka na Kuziangusha Mamlaka ni Mungu, kwa njia zozote mwanadamu hawezi bila Mungu.
MUNGU BARIKI TANZANIA - TIMIZA KUSUDI LAKO KWA WATANZANIA - KATUONDOLEE UOVU - KILA ALIYESHIKA MAMLAKA UKAMTIISHE AKAWE CHINI YA MAMLAKA YAKO - VIONGOZI WOTE UWABARIKI NA KUWAPA HEKIMA YA KUONGOZA TAIFA LA TANZANIA KWA WAKATI ULIO AMRIWA.
Na Ev. Eliezer Mwangosi - Tel. 0767210299 - Email. eliezer.mwangosi@yahoo.com.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment