Thursday, January 07, 2016

Fungu Kuu: “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni milli yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Warumi 12:1
Mapendekezo ya Utaratibu wa Kipindi cha Maombi
Kusifu (kama dakika 10)
• Anzeni kipindi cha maombi kwa kumsifu Mungu jinsi alivyo: Yeye ni mwaminifu, Yeye anajua yote n.k.
• Msifu Mungu kwamba amesubiri kwa muda mrefu ili wewe uweze kumpatia moyo wako wote.
• Mshukuru Mungu kwamba haitaji tu sehemu yako lakini anakuhitaji wewe na talanta zako zote na mapungufu yako.
• Msifu Mungu kwa namna ambazo anakufundisha kukaa ndani Yake.
Kuungama na Kudai Ushindi dhidi ya dhambi (kama dakika 5)
• Muombe Mungu akuonyeshe dhambi ambazo unahitaji kuziunganma kwa uwazi na zile unazohitaji kuziungama faraghani. Dai ushindi juu ya dhambi hizo.
• Muombe Mungu msamaha kama hukuwa ukisalimisha maisha yako kila siku Kwake?
• Muombe Mungu msamaha kwa nyakati ambazo ulitumia muda wako, pesa na talanta kwa ajili yako mwenyewe na si kwa ajili Yake na kwa utukufu Wake.
• Mshukuru Mungu kwamba anakusamehe kulingana na 1Yohana 1:9.
Sala na Maombezi (takribani dakika 35)
• Muombe Mungu aondoe cho chote kile ambacho ambacho kinakuzuia kusalimisha muda, fedha, nguvu, uwezo, hofu na nia yako. Mwambie Mungu unataka kumilikiwa kikamilifu na Kristo.
• Muombe ili Mungu akusaidie kuomba kama Yesu, “walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke” (Luka 22:42)
• Je kuna jambo lo lote linalokuzuia kumpa Yeye uhai wako na moyo wako wote? Mwambie Yeye mambo hayo. Muombe akufanye uwe radhi kuyasalimisha Kwake.
• Omba kwa ajili ya wanafamilia yako na marafiki ambao hawajajitoa kikamilifu kwa Kristo. Muombe awafanye wawe wawe radhi kusalimisha uhai wao Kwake.
• Omba kwamba mchungaji wako wa mtaa na viongozi wa kanisa katika ngazi zote watoe maisha yao yote kwa Mungu.
• Omba kwa ajili ya vijana wa kanisa letu kupata furaha katika kusalimisha maisha yao kwa Kristo na kumfuata. Wainue vijana wa kanisa lako kwa majina yao kupitia kwa maombi.
• Omba kwamba kila kiongozi wa kanisa duniani ashikilie kwa kina mtazamo wa kiroho na wa kiinjilisti. Msihi Bwana awalinde wachungaji na washiriki dhidi ya kupoteza utambulisho wa jinsi tulivyo kama Kanisa la Waadventista Wasabato, kanisa la masalio la Mungu katika kipindi cha mwisho.
• Utume Katika Miji Mikuu – Omba kwa ajili ya Divisheni ya Trans-Europian na miji wanayojitahidi kuileta kwa Kristo: London, Zagreb, Tallinn, Dublin, Copenhagen, Helsinki, Budapest, Bergen, Randstad, Warsaw, Belgrade, Gothenburg, omba kwa ajili ya watu kupata njaa kali kwa ajili ya neno la Mungu.
• Omba ili kwamba watu saba au zaidi katika orodha yako waone hitaji lao na kufungua mioyo yao kwa Roho Mtakatifu.
• Omba kwa ajili ya mahitaji binafsi uliyo nayo.
Shukrani (takribani dakika 10)
• Mshukuru Mungu kwamba atajibu kulingana na mapenzi Yake na kwa wakati Wake.
• Mshukuru Mungu kwamba yupo tayari kuchukua moyo wako wenye dhambi na kuufanya kuwa safi na mtakatifu.
• Mshukuru Mungu kwamba Yesu alikuwa tayari kuishi na kufa, sio kwa ajili Yake lakini kwa mapenzi yake Yule aliyemtuma.
• Mshukuru Mungu kwa kujifunua kwa namna ya pekee katika maisha yako kwatika kipindi hiki cha siku kumi.
Mapendekezo ya Nyimbo
“Tawala Ndani Yangu” no 147, “Nina Haja Nawe” no.126, Univute Karibu” no 148, “Yote Namtolea Yesu” no 122, “Karibu Sana Univute no. 33.
UHAI WETU- ZAWADI YETU KUU KWA MUNGU
“Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni milli yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Warumi 12:1
Kristo aliwafundisha wanafunzi Wake kwamba kiwango cha uangalifu wa kimbingu kwa kitu cho chote huwa sawia na kiwango cha jukumu lililopo kwa kitu hicho katika uumbaji wa Mungu. Kristo alivuta usikivu wa wanafuzi wake kwa mfano wa ndege wa angani. Hakuna shomoro, alisema haanguki chini asipojua Baba wa mbinguni. Na kama ndege huyo mdogo hutambuliwa na Mungu, kwa hakika roho za wale ambao Kristo aliwafia ni za thamani mbele Zake. Thamani ya mtu, kiwango ambacho Mungu anakiweka juu ya mwanadamu, hufunuliwa katika msalaba wa Kalvari. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Je Mungu hatawahukumu wale ambao wanasababisha maumivu au huzuni kwa wale ambao Kristo alitoa uhai Wake kwa ajili yao? Hivyo wanadamu sasa wawe waangalifu kwa namna ambavyo kwa maneno au matendo wanawasababishia watoto wa Mungu huzuni na majonzi.
Kristo alitoa kafari kamili kwa niaba yetu, pale alipojitoia mwenyewe kama sadaka ya dhambi na anatutaka sisi kujitoa kikamilifu Kwake, Yesu anahitaji moyo wote; hatapokea pungufu ya upendo usiogawanyika. “Mungu ni Roho, na wote wamwabuduo wamwabudu katika roho na kweli.
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. (1Wakorintho 6: 19,20)
Iwe tunajitoa kwa Mungu au la, sisi ni Wake. Ninyi si mali yenu wenyewe; mlinunuliwa kwa thamani. Sisi ni mali ya Bwana kwa uumbaji na sisi ni mali Yake kwa ukombozi. Hivyo hatuna haki ya kufikiria kwamba tunaweza kufanya vile tupendavyo. Yote tunayoshikilia ni mali ya Bwana. Hatuna haki sisi wenyewe kwa jambo lo lote, hata kuwepo haipo. Fedha zako zote, wakati na talanta vyote ni mali ya Mungu na vimeazimwa kwetu na Yeye ili kwamba tukamilishe kazi ambayo ametupatia. Ametupatia agizo, “Fanyeni biashara hata nitakapokuja”
Upendo wa Kristo katika moyo ndicho kinachohitajika. Ubinafsi wapaswa kusulubishwa. Wakati ubinafsi unapozamishwa katika Kristo, upendo wa kweli utatiririka kwa uhiari. Sio hisia wala msukumo lakini uamuzi nia iliyotakaswa. Haipo katika hisia lakini katika kubadilishwa kwa moyo wote, roho na tabia, ambayo imefia nafsi na kuishi kwa ajili ya Kristo. Bwana wetu na Mwokozi wetu anatuhitaji tujitoe Kwake. Kusalimisha ubinafsi wetu kwa Mungu ndiyo yote anayohitaji, kujtoa kwake kutumika kama apendavyoYeye. Ni hadi tutakapofika katika hatua hii ya kujisalimisha, ndipo tutaweza kufanya kazi kwa furaha, kwa faida na kwa mafanikio po pote pale.
Mbele yangu leo ninaona wale ambao Mungu anaweza kuwatumia kama watamtegemea Yeye ….Ni heshima kumfuata Mwokozi. Na ni kwa kutii maagizo aliyotoa kwamba utaandaliwa kwa ajili ya kukutana Naye pindi ajapo. Kama utamwomba Mungu akusaidie kushinda tabia isiyo ya Kikristo katika mwenendo wako, atakuandaa kwa ajili ya kuingia mbinguni, mahali ambapo dhambi haiwezi kuingia. Wale ambao kila siku wanatoa maisha yao kwa Kristo, na wale ambao wanatafuta kumjua, watabarikiwa sana. Sema hivi, Kristo alitoa maisha Yake kwa ajili yangu, nami lazima nitoe maisha yangu Kwake. Kama utajitoa kikamilifu Kwake, utakuwa mshindi katika vita dhidi ya dhambi. Bwana Yesu Kristo atakuwa msaada kwako, atakuwa mdhamini kwako, nguvu zako kama utampokea na kumtii Yeye.
Katika kisa, lulu haitolewi kama zawadi. Mfanyabiashara aliinunua kwa gharama ya vyote alivyokuwa navyo. Maswali mengi juu ya hili, Kristo anaelezewa katika Maandiko kama zawadi. Yeye ni zawadi, lakini kwa wale tu ambao wanajitoa wenyewe, nafsi, mwili na roho, mwili, kwake bila kuzuia cho chote. Tunapaswa tujitoe wenyewe kwa Kristo, kuishi maisha ya utii wa hiari kwa matakwa Yake yote. Vile vyote tulivyo, talanta zetu na uwezo wetu tulio nao ni vya Bwana, kuwekwa wakfu kwa huduma Yake. Tutakapojitoa kikamilifu Kwake, Kristo pamoja na hazina zote za mbinguni, hujitoa mwenyewe kwetu. Nasi tunapata lulu ya thamani.
Maswali ya Kujitathmini
1. Wewe ni wa thamani sana mbele za macho ya Mungu kiasi kwamba alifanya yote kukufanya uwe Wake. Hili hukufanya ujisikieje?
2. Fikiri juu ya kile ambacho Yesu alikupatia ili mbingu iwe yako. Je inakstahili kujitoa Kwake kila siku? Je hilo siyo jambo la msingi zaidi kufanya?
Stephen Letta's photo.



****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA