Friday, January 08, 2016

Tafakari: Waefeso 6:11 "Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani".
Neno hila linaweza kueleweka vizuri kwa kutumia mfano wa wavuvi wa samaki, ambao wakitaka kumnasa samaki mkubwa kwa kutumia ndoano, wanaweka dagaa kwenye ndoano au wegine wanatumia vibati vidogo vinavyong'aa kwenye maji na kuonekana kama samaki mdogo. Mara zote samaki wakubwa wamenasa kwenye ndoano wakiwa wanameza samaki mdogo ambaye kwa ndani kuna ndoano. Mvuvi ametumia HILA kumnasa samaki kwa ulaghai wa kuweka doano ndani dagaa ili kumnasa samaki mkubwa.
Mtandao ni moja ya mtego hatari ambao shetani anautumia siku hizi kuwanasa vijana kwa wazee, wengi wamekuwa ni marehemu, waliokufa kiroho kwa sababu ya mitandao. Nakumbuka zamani wazazi wenye maadili walikuwa wanawakataza vijana wao wasiende kwenye majumba ya dansi na sinema, kwa kuogopa kuharibika tabia, katika kizazi hiki, majumba ya dansi na video hadi za ngono ziko mikononi na majumbani.
Siku hizi mahusiano mengi, hadi ya uchumba huanzia kwenye mtandao, udanganyifu mwingi unatendeka kwenye mitandao na wengi wananasa bila kujua, mvulana mmoja alipoteza muda mwingi wa uchumba na bibi kizee wa miaka 70 aliyekuwa ameweka picha yake ya urembo akiwa msichana kwenye Facebook. Wee kazana tu ku type "cuteee" mara "Sweetee" kumbe ni mwanaume kaweka picha na jina la mrembo kwenye profile yake, mtadanganywa hadi lini?.
Uchumba hadi ndoa vinavunjika kutokana na vijana wengi kuharibikiwa akili kwa sababu ya mazoea machafu kupitia mitadao. Utakuta vijana wanajisifia kwa kufanya ngono za mtandaoni (sex online), na wapenzi wao wanaofahamiana kwa picha, shetani ametega nyavu kwenye mtandao, roho chafu za mahaba zinawaunganisha wanaume kwa wanawake, ili wote wachafuliwe akili na kupagawa na mapepo ya Ngono. Mitandao imekuwa ni bahari yenye kubeba uchafu wa kila namna unaoifunika dunia yetu.
Vijana wengi wanapoteza muda kwa ku chat, mara FB, WhatsApp, twitter, instagram, imo, etc, ukifuatilia anachokifanya ni ku like ujumbe hata bila kuusoma na kuangalia picha au video. Kizazi hiki kinaendelea kujeruhiwa kwa vijana kutokuwa makini na masomo bila kusahau uzembe kazini. Muda mwingi unapotea ukitumika ku peruzi mambo yasiyo na tija katika maisha, wengi wanapoteza muda na mwisho inawagharimu.
Hata hivyo kwa upande mwingine mtandao ukitumika vizuri, una faida kubwa sana kwa maisha ya binadamu, neno la leo lisingewafikia wengi na kwa haraka pasingekuwepo mtandao. Ndio maana tafakari ya leo, inatujulisha jambo la kufanya ili mtandao uwe na faida kwetu kuliko hasara ambayo wengi wanaipata. Tunapaswa kuvaa silaha za Mungu ili tuweze kuzipinga HILA ZA SHETANI za kwenye mitandao. Silaha za Mungu ni kuruhusu uongozi wa Roho mtakatifu kutawala akili zetu daima.
MUNGU ATUJALIE HEKIMA NA MACHO YA KUONA MITEGO YA SHETANI KUPITIA MITANDAO.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE KUJAA MAFANIKIO NA BARAKA TELE
Na Ev. Eliezer Mwangosi - Simu: +255(0)767210299


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA