Friday, January 15, 2016



Viongozi mbalimbali wa dini

 Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (wa pili kushoto walioshikilia bendera), katika Maombi ya Kumuombea Rais Magufuli na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza. Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza kwa kushirikiana na Umoja wa Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam jana January 13,2015 ulifanya Maombi Maalumu ya Kumuombea Rais wa wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake. 
Maombi hayo yalifanyika katika Uwanja wa Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali na Dini huku pia wananchi wakijumuika pamoja na waumini wa dini mbalimbali katika maombi hayo. Mgeni Rasmi katika maombi hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae katika hotuba yake, aliwasihi Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa ili kuondokana na vikwazo mbalimbali ambapo alidokeza kuwa kupitia maombi kama yaliyofanyika jana, migogoro mbalimbali ikiwemo ya kisiasa kama iliyopo Zanzibar itamalizika. Viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Askofu Charles Sekelwa, Makamu wake Zenobius Issaya pamoja na Kiongozi wa Kundi la Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam la Good News For all Ministry Askofu Dr.Charles Gadi pamoja na viongozi wengine wa dini kutoka mikoa mbalimbali nchini waliliombea Taifa na kuhimiza utulivu nchini. 
Pamoja na mambo mengine, ia maombi hayo yalijumuisha toba kwa taifa, kumuomba Mungu kukomesha mauaji ya Vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na kuombea taifa mvua zisizo na madhara. 






Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akizungumza katika Maombi ya kumuombea Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.





Picha/Habari na Mtangazaji Maduhu
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA