Friday, January 15, 2016

Tafakari: Ufunuo 2:10 "Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. UWE MWAMINIFU HATA KUFA, nami nitakupa taji ya uzima".

Unabii huo ulikuwa juu ya kanisa la Kristo amgbalo katika nyakati mabalimbali limepitia mateso, hadi wengine kufikia kifo kwa ajiri ya Kristo. Hata leo tunashuhudia shetani akiwaangusha wengi katika majaribu na vitisho, na wengi wanaishia kuanguka na hatimaye kufa bila tumaini la uzima wa milele. 

Je ni wangapi wapo tayari kupata hasara ya maisha haya kwa ajili ya msimamo wao kwa Mungu? Mara nyingi shetani anageuza mambo, anawaletea vijana wa kike na wa kiume, na watu wazima, mambo ambayo yanaonekana yanafaida katika maisha haya, wakati kwa vipimo vya Mbinguni ni Uovu unaoleta majuto milele. 

Nilisikia binti aliyekuwa amefumaniwa na mume wa mtu, akidai hawezi kumuacha, kwa sababu hana njia nyingine ya kuishi. Na wengine utasikia, "wanaume wa siku hizi hawaoi bila kukujua kimwili - zinaa", hata hivyo ndio kwanza tunashuhudia wachumba wanabwagwa kila kukicha. 

Vijana kwa wazee wanazidi kujeruhiwa na muovu shetani kwa udanganyifu wa kupata faida katika maisha ya dhambi, na mwisho wa yote wanaishia kutengwa na Mungu wao. Hata viongozi wa Dini wengi wanaishia kupotea kwa kujitafutia makundi kwa njia hata ya undanganyifu ili wapate fedha za kuendeshea maisha. Uizi, udanganyifu, utapeli, uongo ni tabia za kawaida maofisini, katika mahusiano, kwenye biashara, vyuoni n.k. Watu sio WAAMINIFU. 

MUNGU ATUSAIDIE TUWE WAAMINIFU DAIMA, TUWE TAYARI KUFA KULIKO KUMKOSEA MUNGU.

MUNGU AWAPATIE SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE

Ev. Eliezer Mwangosi - Simu: 0767210299

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA