Magreth - mama anayejitambua kama Nabii, ametokea akidai ana ujumbe
aliopewa na Mungu kuwaonya wanawake (hasa wakristo) wasivae nguo
zinazoonesha uchi bali wavae nguo kama hiyo aliyovaa yeye (pichani
kulia). Nilikutana na Magreth alipokuja kwenye semina ya uongozi
iliyokuwa inahitimishwa leo hapa Mwenge ili aonane na viongozi wa
Konferensi na Union awaambie kile Mungu alichomwagiza kwao. Hapa
anajaribu kujibu maswali kutoka kwa mmoja wa wanasemina ndugu Mduma -
dereva wa Mwenyekiti wa Union. Magreth ni mwaadventista anayesali huko
Kipunguni Ukonga. Ingawa anaonekana kukiamini kwa dhati (conviction)
hicho anachokiita mafunuo bado anahitaji msaada ili afahamu asili ya
hiyo nguvu iliyo nyuma yake. Tumuombee
chanzo Stephen Letta
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
chanzo Stephen Letta
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***




0 comments:
Post a Comment