Sababu za kuchelewa kuchumbiwa
Zipo sababu nyingi zinazofanya wasichana wachelewe kuchumbiwa. Hapa nitazungumzia baadhi ya sababu za kujitakia
zilizopelekea baadhi ya wasichana kujikuta wakichelewa kuchumbiwa.
Wasichana wengine kwa kujichukulia kuwa wao ni wazuri sana na wana soko, wamekuwa wakiwakataa wavulana
wanaowaulizia uchumba hata pale wanapokuwa wamekidhi vigezo kwa mataraji ya kumpata mwenye vigezo vya juu
kuliko wengine wote.
Wengine huwakataa wachumba kutokana na shinikizo la wazazi wenye kutaka mvulana mwenye uwezo wa kiuchumi
au wa kabila lao. Wakiwa na matarajio kuwa wachumba wataendelea kuja ghafla hushangaa kuona idadi ya
wachumba ikipungua na kugundua kuwa soko lao limeshuka jambo linalowaweka kwenye wasiwasi wa kukosa
wachumba wa kuwaoa.
Wengine hukutwa na janga la kutochumbiwa kutokana na kutumia kejeli na lugha za kashfa katika kuwakataa
wachumba wanaowajia na hivyo kuchukuliwa kuwa ni msichana mwenye dharau jambo ambalo karibu wavulana wote
hukerwa nalo.
Wengine huchelewa kupata mchumaba kutokana na kujiweka katika mazingira ya soko la nje zaidi kuliko soko la
ndani. Maana yangu hapa ni kuwa msichana anayejiremba na kuvalia kama watu wa duniani hawezi kutarajia kupata
wavulana wa kanisani wamuulizie uchumba.
Wengine huchelewa kupata wachumba kutokana na kutojiweka wazi kuwa wanahitaji mchumba na kutokuwa karibu
na yule wanayevutwa naye kuwa mchumba wao.
Sababu nyingine ya kuchelewa kuchumbiwa ni tuhuma zilizozagaa zingine zikiwa za kweli na zingine zisizothibitishwa
kwamba binti au mvulana fulani ana tabia mbaya. Mabinti wengine wamezushiwa kuwa ni malaya eti tu kwa sababu
ana mazoea na wavulana bila kujua kuwa wapo wasichana wanaofanya hivyo si kwa sababu ya umalaya. Wapo
waliotuhumiwa kuwa ni walevi, wezi, wavutaji kwa sababu tu ya makundi wanayoshirikiana nayo. Kama watu
wamekutuhumu kwa lolote baya na unajua hiyo itakuharibia sifa yako jitulize. Kama tabia hiyo unayo tubu na kwa
msaada wa Mungu iache tabia hiyo. Na kama ni kwa sababu ulizalia nyumbani endelea kumlilia Mungu wako ili
wanaokulaumu watambue ulifanya kwa ujinga na ya kuwa unajutia kitendo hicho na kwamba Mungu amekusamehe.
Usigombane na watu. Wewe endelea kumtumaini Mungu naye atakupa haja za moyo wako.
Uchumba uliokidhi vigezo
Kuoa au kuolewa ni jambo nyeti sana linalohitaji umakini kulipangilia. Ukihisi umefikia wakati unaohitaji kupata mchumba
utakayefunga naye ndoa, chukua tahadhari kubwa. ?Uangalifu mkubwa ni lazima ufanyike na vijana wa Kikristo katika
kuunda urafiki na katika kuchagua mwenzi wa maisha. Uwe macho, isije ikawa kile ukidhaniacho kuwa ni dhahabu
kikageuka kuwa chuma cha kawaida.? (Adventist Home uk. 45)
Hakikisha umemshirikisha Mungu kwa kila hatua ya uchumba. Usikurupuke ukamvamia asiye wako. Mungu wako anakujali
na amekuandalia mtu mtakayechukuliana naye. Unachotakiwa ni kumwomba kwa dhati akuoneshe mwenzi aliyekuchagulia.
Kumbuka mke mwema mtu hupewa na Bwana. Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima
cha marijani.? (Mithali 31:10) ?Katika hali ya kawaida ni jambo gumu kumpata mume au mke mwema. Wengine hujikuta
wakiambulia waume na wake ambao hawakuwatarajia maishani. Kwa nini? Hawakumwalika Mungu. Mungu anakuomba
umshirikishe ili akusaidie kupata mwenzi mwema.
Angalia ahadi za Mungu kwa wanaomtumainia. ?Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye
busara, mtu hupewa na Bwana.? (Mithali 19:14). ?Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na
utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.? (Zaburi 84:11). ?Nawe utajifurahisha kwa Bwana, Naye
atakupa haja za moyo wako.? (Zaburi 37:4).
Kigezo cha mchumba afaaye:
1. 1. Chagua Anayempenda Mungu:
Kigezo nambari moja cha mchumba anayefaa ni yule anayemheshimu Mungu. Yule asiyemheshimu Mungu atakuwa
kikwazo katika ndoa na matarajio yako. Ndoa huundwa na watatu. Ninyi wawili kwa upande mmoja na Mungu kwa upande
mwingine. ?Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha
bure.? (Zaburi 127:1). Ikiwa mmoja wenu hana mahusiano na Mungu ni dhahiri safari yenu ya ndoa mtakuwa mmeianza
vibaya. Ni lazima kuanza na Mungu katika hatua ya uchumba na kuendelea na Mungu katika kipindi chote cha ndoa
vinginevyo muunganiko huo badala ya kuwa mbaraka utakuwa laana. Ikumbukwe ndoa si kitu cha majaribio kwamba baada
ya kugundua uliyefunga naye ndoa hafai unaweza kuvunja na kuanza upya. ?. . . Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu
asiwatenganishe.? Mathayo 19:6.
Ni lazima unayeunganishwa naye kwenye ndoa awe unayefanana naye, hasa katika maswala yanayohusu imani. Mungu
aliye mwasisi wa ndoa, alipomtafutia Adamu mchumba alimtafutia anayefanana naye. ?Bwana Mungu akasema, Si vema
huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.? (Mwanzo 2:18). Ni wazi kuwa wasiofanana hawawezi
kutembea pamoja. ?Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?? (Amosi 3:3). Hali kadhalika
mpagani hawezi kwenda njia moja na Mkristo. Mungu anawaagiza vijana na watu wazima kutooana na wasio wa imani moja
nao. ?Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi?
Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza.? (2 Wakorintho 6:14).
Walio kwenye imani moja husaidiana kiroho walio imani tofauti hupingana. ?Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana
wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke
yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!? (Mhubiri 4:9-10). Aliyeoana na asiye wa imani moja naye ni kama
aliye peke yake. Atakuwa na wakati mgumu kuilinda imani yake. Vijana wa Kiadventista mnahimizwa kuoa na kuolewa na
wenzenu waliopo kanisani. Msijaribiwe kuoa huko nje, waliojaribu kufanya hivyo wamefikwa na matatizo mazito ya
kuhuzunisha na sasa wanajutia maamuzi waliyoyafanya ujanani.
1. 2. Chagua unayempenda
Kigezo cha pili muhimu cha mchumba anayefaa ni yule unayempenda. Kupenda kunakokusudiwa hapa si misisimko au
mihemko inayosukumwa na tamaa za mwili bali ni upendo halisi utokao moyoni unaomkubali mtu jinsi alivyo. Yule ambaye
Mungu amekuchagulia utamtambua kwa kuona upendo ndani yake; upendo unaokuelekea wewe ukiwa na makusudi ya
dhati, ya kudumu, na yasiyofichika. Upendo huo siyo mpofu usioruhusu akili kuchambua na kujiridhisha. Ni upendo usio na
haraka, usiolazimisha na usiotafuta faida zake wenyewe. ?Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo
hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii
udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.? (1 Wakorintho
13:4-7.
Usijilazimishe kuoana na usiyempenda ama kwa sababu ya kumhurumia, kwa sababu ya kuwaridhisha watu fulani au kwa
sababu ya kutafuta faida fulani tu. Viapo vya siku ya ndoa vimewekwa ili kuthibitisha kama mnaoana kwa hiari mkisukumwa
na upendo peke yake. Zimekuwepo siku hizi ndoa zinazodumu kwa muda mfupi kama hiyo moja niliyowahi kufunga
iliyodumu kwa chini ya mwezi mmoja. Inakuwa kama watu wanafanya mzaha na ndoa. Vijana acheni kutafuta sifa ya kuwa
mmefunga ndoa na kumbe mna mpango wa kuachana baada ya muda mfupi. ?Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi
yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.? (Waebrania 13:4).
1. 3. Vigezo vingine muhimu vya mchumba afaaye:
Mchumba akiwa anampenda Mungu na wewe mwenyewe uwe pia unampenda huyo mchumba hiyo inatosha kukuhakikishia
kuwa yeye ni mchumba mwema mradi Mungu awe amekuonesha kuwa huyo ni wako. Kutegemea ndoto au ishara katika
kumtambua mchumba ambaye Mungu amekuchagulia si salama katika kizazi hiki cha udanganyifu. Mahusiano yako ya
karibu na Mungu, yanatosha kukufanya umfahamu yule aliye wako hasa. Vigezo vingine vya kimo, kabila, utaifa, rangi,
elimu, umri, hali ya kiuchumi na kadhalika si muhimu sana katika kuamua mchumba afaaye ingawaje wakati fulani huweza
kusaidia. Hata hivyo inashauriwa tofauti ya mambo hayo isiwe kubwa kiasi cha kuathiri maelewano na ukaribu katika ndoa.
Washirikishe watu makini wenye kukutakia mema
Swala zito kama uchumba linahitaji kushirikisha watu makini wenye kukutakia mema. Wajulishe wazazi na kuwauliza
ushauri wao. pima ushauri wao na kama unalingana na mashauri ya Mungu uuchukue. Viongozi wa kanisa, marafiki na
jamaa wengine utakaowahusisha hakikisha wana sifa ya kuwa watu makini wenye kukutakia mema na wamchao Mungu.
Itakapotokea ushauri wa watu hao unapingana na maagizo ya Mungu chukua tahadhari. Mshirikishe zaidi Mungu kwa kuwa
na maombi ya dhati ya mara kwa mara huku ukichukua hatua ya kufunga katika siku kadhaa. Mungu atakuelekeza cha
kufanya katika kila hatua hata kama kuna magumu yanaweza kujitokeza.
1. 1. Nini kifanyike ili kuepuka makosa ya kuchagua mchumba asiyefaa?
2. 2. Nini kifanyike kupunguza wimbi la vijana wetu kuoana na wasio wa imanni moja nao?
3. 3. Ni muda upi ufaao kuanza kutafuta mchumba?
4. 4. Kipindi cha uchumba kinatakiwa kisizidi na kisipungue muda gani?
5. 5. Je ni muhimu kupima afya na mchumba wako ili kujua kama ameathirika?
6. 6. Je ni vizuri kumwacha mchumba baada ya kuthibitika ameathirika?
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:
Post a Comment