Sunday, February 14, 2016

(13 Februari 2016)
Somo hili limeandaliwa na Willie Na Elaine Oliver (Wakurugenzi wa Idara ya Huduma za Familia wa Konferensi Kuu na kuratibiwa na Dr Josiah Tayali, Mkurugenzi, Idara ya Huduma za Familia wa ECT.
FUNGU KUU: LUKA 9:23-24
“Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”.

SOMO LA WATOTO:
KICHWA CHA SOMO: MMISHENARI KWA AJILI YA YESU.

Maandalizi ya awali kabla ya somo:
Andaa picha ya sura ya mtoto mwenye furaha; tengeneza mataji kwa kutumia karatasi ngumu, au wiki moja kabla ya somo muombe kila mzazi ahakikishe mtoto wake anakuja na taji aidha iliyotengenezwa au kununuliwa nawe uwe na taji yako pia. Hakikisha kila mtoto ana Biblia yake na kama hana akachukue kwa mzazi kabla hujaendelea na somo. Waombe wote wasome kanuni ya mbingu katika Biblia zao Kama ilivyoainishwa katika kitabu cha Mathayo.

KANUNI YA MBINGU; Mathayo 28:19-20
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”
WIMBO
Waombe watoto waimbe wimbo ufuatao kwa vitendo [huu ndio muda muafaka wa kuvaa taji] jifunze wimbo huo kabla ya somo. “Nitavaa taji nyumbani mwa baba, nyumbani mwa baba, nyumbani mwa baba, Nitavaa taji nyumbani mwa baba ni furaha, furaha, furaha.”

Kisa- [Waombe watoto wenye umri wa Miaka 8 wasimame ili muwatambue kama vielelezo vya kisa cha somo la leo, kisha wakae.]!
Mtoto mdogo anayeitwa Petro mwenye umri wa miaka nane, alikua na furaha kujua kuwa Yesu anampenda na kwamba siku moja atamvika taji akiishaifanya kazi kubwa ya kuwahubiri wengine kama ilivyo kanuni ya mbingu. Kanuni hiyo ni ipi?
[Waombe watoto warudie kusema fungu la; Mathayo 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa Dahari].
Moyo wake mdogo ulijawa na shauku kutaka kuwaeleza wengine habari za Yesu. Hivyo basi akamuomba baba yake ruhusa ya kuanzisha darasa la kujifunza NENO la Mungu. Baba yake alifurahia jambo hilo na kumtia moyo. Kesho yake mtoto Petro akiwa amejaa uso wa furaha [onyesha picha ya uso wa mtoto mwenye furaha] alitembea mtaani akiwaalika watoto wenzake kujifunza neno la Mungu pamoja naye nyumbani kwao kila Jumatano jioni. Siku ya kwanza walikuja wachache lakini miezi iliposogea walikua wengi zaidi ya kumi na Petro aliwaambia kuhusu mji wa mbinguni na anavyotamani wote waende mbinguni kasha aliimba pamoja nao na kuwafundisha neno la Mungu. [Imba tena wimbo wa Tutavaa Taji………. kwa vitendo pamoja na watoto].
Baada ya miezi michache watoto kumi walibatizwa na kujiunga na kanisa la Waadventista wa Sabato. Hivi sasa waumini wameanza kupatikana lakini hakuna kanisa la kuabudia, na hivyo Petro alimwendea mchungaji na kumuomba wafanye utaratibu wa kujenga kanisa. Hakuna ambaye angeweza kuizima roho ya umishonari iliyokuwepo ndani ya mtoto Petro. Wakati fulani alifunga na kuomba kwa ajili ya ujenzi wa kanisa. Shule zilipokua zimefungwa Petro alitembea huku na kule akichangisha pesa kwa ajili ya jengo la kanisa. Alijitoa mhanga kwa ajili ya kazi ya Mungu. Aliamini Mungu atafungua njia mpaka jengo lijengwe.

Waulize watoto: - Wangapi wamewahi kufunga na kuomba? Watie moyo kwamba hata wao wanaweza kufunga na kuomba kwa ajili ya jambo lolote na Mungu akajibu.
Hatimaye jengo likaanza kujengwa na Petro alipokua amerudi kutoka shule alienda katika eneo la kanisa jipya na kusaidia kusogeza matofari. Hakika Mungu alimtumia Petro kama mmishonari mdogo wa kupeleka watu mbinguni ambako tutaishi milele na kuvaa taji. Baada ya miezi mingi kanisa lilikamilika na watu walimtukuza Mungu kwa namna ambavyo alimtumia mmishonari mdogo huyu kuwaleta watu kwa Yesu na kujenga kanisa. Petro aliendelea kuwahubiri watu kwa zaidi ya miaka mitatu na hata kuwaambia wanafunzi wenzake darasani habari ya marejeo ya Yesu yaliyokaribia sana na kuwataka wajiandae ili wakavikwe taji nyumbani kwa baba.

Mwezi wa sita tutakuwa na effoti ya watoto kule Masasi, wangapi wanatamani kuwa wamishonari wadogo kama Petro? Anza sasa kuwashuhudia watu wengine habari za Yesu pia ukienda nyumbani ombea mkutano mkubwa huo wa kule Masasi ili wengi wavutwe kwa Yesu nanyi mpate kuvikwa taji mbinguni baada ya kazi. Mungu awabariki sana. [Imbisha tena wimbo wa Tutavaa Taji……. huku ukipepea picha ya uso wa mtoto mwenye furaha.]
Hitimisha kwa ombi la kuwaombea wamishonari wadogo waliojitoa kwa Yesu siku hiyo. Watie moyo wazazi wawasaidie watoto kufanya uinjilisti.
KICHWA CHA SOMO: MSALABA NA NDOA ZA KIKRISTO.
UTANGULIZI
Mara nyingi watu hufurahia kula chakula, na hasa wakiwa wamepata vionjo mbalimbali baada ya kusafiri na kutembelea maeneo mbalimbali. Tatizo linakuja baada ya kurudi nyumbani ni ladha ipi uweze kuitumia maana ladha zote ulizokutana nazo ni nzuri. Kufanya maamuzi hayo hujumuisha nini cha kufanya na ndoa zetu kwa wakati huo. Somo letu la leo lina kichwa kisomekacho;” NDOA ZA KIKRISTO NA MSALABA”. Tuombe.

Maisha Ya Kujikana Nafsi;
Luka 9:23-24; Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.

Katika Injili ya Luka Sura ya 9, Tunakutana na Yesu na wanafunzi wake wakiwa kazini wakikemea mapepo na kuponya wagonjwa. Ni wakati huo ambapo Yesu anatuma wanafunzi wake waende wakahubiri habari njema ya injili huku akisikiliza uzoefu wao wa kufurahisha wa kazi ya utume. Yeye alikuwa amemaliza tu kufanya miujiza ya kuwalisha watu elfu tano katika maeneo ya nje ya Bethsaida.
Baada tu ya maombi, Yesu anarudia mazungumzo yake na wanafunzi wake akiomba taarifa juu ya kile watu wasemacho juu yake. Wengine walisema kuwa Yesu ni Yohana mbatizaji aliyefufuka kutoka katika wafu wakati wengine walisema ni Eliya. Pamoja na hayo Yesu alitamani kujua wanafunzi wake wanasema nii juu yake. Petro akajibu swali hilo kwa kusema ‘Wewe ndiwe Kristo wa Mungu.’
Mazungumzo haya yalikua yanafafanua sababu za ujio wa Yesu duniani, na pia kudhihirisha nguvu waliyopokea wanafunzi wa Yesu na kushuhudia muujiza wa ajabu waliouona kwa macho yao, ule wa kuwalisha watu, sio kwa sababu ya ubinafsi au majivuno bali kuwaonyesha binadamu waliopotea UPENDO na kujali mahitaji yao ya kila siku. Sababu kuu ya kuja kwa Yesu ni kufanya maisha haya yaliyoharibika kuwa ni ya mibaraka ya aina yake.

SOMA ZAIDI HAPA 





****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA