Tafakari:
Hesabu 13:30-32 "Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, na
tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Bali
wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, hatuwezi kupanda tupigane na
watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea wana wa Israeli
habari mbaya......."
Kisa
hiki kinapatikana Hesabu sura 13 hadi 14 yote, Bwana aliwatuma wajumbe
12 kwenda kuipeleleza nchi ya Kanani na kuleta taarifa kwa Israeli,
hatimaye waanze safari ya kwenda na kuweka makao huko. Taarifa iliyokuja
ilikuwa na sura mbili; 1. Ilikuwa nchi nzuri yenye maziwa na asali, 2.
Ilikuwa inchi yenye watu wa kutisha na ngome isiyoingilika.
Wajumbe
10 wakatoa habari mbaya ya kutisha hadi kuwafanya waisraeli wavunjike
moyo, wakaanza wote kuomboleza kwa kuogopa kuuwawa. Hata hivyo Kalebu na
Yoshua wakasimama kinyume nao wakisisitiza kuwa, Mungu yupo
atawashindia vita na kuwaangamiza maadui. Mwishowe wakaamua kuwaua kwa
kuwapiga mawe Kalebu na Yoshua, ili wao waanze safari kurudi misri, hata
hivyo Mungu aliingilia kati hawakuweza kuwapiga.
Matokeo
ya waisraeli KUWAZA NA KUAMUA VIBAYA juu ya uwezo wa Mungu; walikaa
jangwani miaka 40, na wote waliohusika kumnung'unikia Mungu walifia
jangwani bila kufika nchi ya ahadi, isipokuwa Kalebu na Yoshua, ambao,
japokuwa walikuwa na TAARIFA SAHIHI Juu ya utisho wa majitu ya Kanani,
walidumu kuwa na mawazo na maamuzi sahihi juu ya kumtegemea Mungu.
Wapendwa;
kizazi chetu kimejaa taarifa nyingi na sahihi zinazokatisha tamaa na
wengine kuvunjika moyo. Utasikia watu wakisema; Ugonjwa huu hauna dawa;
Ukoo wenu una laana huwezi kufanikiwa; Umezaliwa huna akili huwezi
kufaulu; Umezidi miaka 35 huwezi kuolewa; Ulipimwa ukaonekana tasa
huwezi kubeba Mimba; Pale kuna chuma ulete huwezi kufanya biashara bila
kuzindika; Ukoo wenu ni maskini hawezi kufanikiwa n.k....
Wengine
utawasikia wakisema; Siku hizi huwezi kupata mchumba mwaminifu; Huyo
mwanaume hawezi kurudi amelishwa limbwata; Huwezi kufaulu bila kutoa
rushwa ya ngono; Huwezi kuishi bila kutenda dhambi..... nk. Wengi wana
taarifa tena sahihi zilizojaa maneno ya, HAIWEZEKANI.... HAIWEZEKANI....
HAIWEZEKANI. Neno la leo linasema KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.
Rafiki;
Inua macho yako juu, tazama na kuamini juu ya ahadi na uwezo wa Mungu.
Achana na mawazo HASI, uwe na mawazo CHANYA ukimtegemea Mungu, naye
atatimiza ahadi zake juu yako.
MUNGU AWAPATIE SIKU NJEMA YENYE AMANI NA MAFANIKIO TELE.
Na: Ev. Eliezer Mwangosi - Simu ya Whatsapp: 0767210299.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
MUNGU AWAPATIE SIKU NJEMA YENYE AMANI NA MAFANIKIO TELE.
Na: Ev. Eliezer Mwangosi - Simu ya Whatsapp: 0767210299.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***



0 comments:
Post a Comment