Friday, February 05, 2016



Kundi moja la watu wasioamini kwamba Mungu yupo linasema kuwa limebaguliwa baada ya serikali kukataa kulisajili.
Liliambiwa kwamba ombi lao lilitupiliwa mbali kutokana na wasiwasi kwamba hatua hiyo itavuruga amani na utulivu nchini.
Msemaji wa chama cha wasioamini Mungu
Wanachama hao walio 60 nchini Kenya waliwasilisha ombi la kutaka kutambuliwa rasmi mwaka jana. Zaidi ya asilimia 97 ya Wakenya wanajitambulisha na dini mbali mbali kulingana na utafiti uliofanywa na Pew.
Mkuu wa wanachama hao nchini Kenya AIK, Harrison Mumia amemshtumu afisa wa usajili Maria Nyariki kwa kuendesha afisi yake kwa kukisia,na kwamba hajui athari za usajili wa kundi hilo.
Ameongezea kuwa kuna viongozi wa makanisa ambao wamewabaka watoto wadogo ,na wameruhusiwa kusajili makanisa yao.
AIK ina haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini Bw Mumia ameiambia BBC kwamba atawasilisha malalamishi hayo katika mahakama, kwa kuwa haki yao ya uhuru wa kushiriki imekiukwa.
                                                  MSIKILIZE HAPA AKIJIELEZA
AIK inaamini kwamba utambulizi rasmi wa kundi hilo utaliwezesha kushiriki zaidi katika maswala ya uma,mbali na kuliwezesha kufanya vitu kama vile kufungua akaunti za benki.
Bwana Mumia amesema kuwa kama watu wasio amini kwamba Mungu yupo katika jamii ya kidini,yeye binafsi amebaguliwa.
Mwaka uliopita AIK ilifeli katika jaribio la mahakamani kubatilisha uamuzi wa serikali kuwa na siku kuu ambayo itakayoambatana na siku ya ziara ya papa Francis nchini Kenya.
BBCSWAHILI


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA