Warumi 12:9 "Pendo na lisiwe na Unafiki; lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema".
Kama kuna changamoto kubwa katika kizazi chetu ni kuupata Upendo wa kweli. Vijana Kwa wazee na wanaume kwa wanawake, asilimia kubwa wanajeruhiwa kwa Upendo wenye Hila na Unafiki ndani yake.
Mabinti na hata akina mama wengi, wamepitia majeraha na kuumizwa na wapendwa waliojifanya wanawapenda, kumbe lilikuwa ni Pendo la Kinafiki na hila. Lakini pia ndivyo ilivyo kwa Wavulana, wengine wamejikatia tamaa hawataki kusikia Mahusiano Kwa jinsi walivyoporwa wapenzi wao na wenye nazo.
Bahati mbaya Sana, hata wanaojiita watoto wa Mungu wanapitia, majeraha haya ya Upendo Feki. Wengi wamejikatia tamaa ya Kuolewa na Kuoa, na wengine wako kwenye ndoa zilizogeuka Ndoano, ni vilio na adha zisizokoma.
Kizazi chetu kwa ujumla kinazidi kupoteza Upendo wa Kweli, kwa sababu KUMCHA MUNGU kunazidi kupotea, wengi wanamrudia Mungu wakiwa tayari ni Majeruhi.
Mtume Paulo, anatoa onyo kwa watoto wa Mungu, wasiotulia na kuhemea kwa Pendo la Unafiki wenye Kujeruhi dhamiri za wenzao, sawa na wakorintho walivyotendeana.
1 Wakorintho:8:12 "Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo".
Ukimkosea mwenzio kwa jambo lolote, unamtenda dhambi Kristo, mwisho wake ni kilio cha kusaga meno. Ni wakati wa kumrudia Mungu wetu, atuepushe na mitego, ili tusinaswe na tusiwe na Upendo wenye Unafiki na Hila.
MUNGU NA AWAPATIE NEEMA YA KUISHI MAISHA YENYE FURAHA NA AMANI.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE.
Na. Ev. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767 210 299.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment