Isaya 54:4 "Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana
hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya
ujane wako hutayakumbuka tena".
Katika ulimwengu huu wa dhambi, mwanadamu anapitia changamoto mbalimbali, ambazo wakati mwingine zinaleta kukosa matumaini na kuvunjika moyo.
Katika ulimwengu huu wa dhambi, mwanadamu anapitia changamoto mbalimbali, ambazo wakati mwingine zinaleta kukosa matumaini na kuvunjika moyo.
Ninaamini hata siku hii ya leo, kuna mtu fulani anapitia changamoto ambayo imedumu kwa mda mrefu bila kupata ufumbuzi.
Bila kujali umejeruhiwa kiasi gani, bila kujali tatizo limedumu muda mrefu kiasi gani, bila kujali uzito wa tatizo lako, hata kama huoni mwisho wa shida yako. Hata ujione umeaibika na watu wanakubeza na dhihaka juu.
Neno la leo linasema, siku yaja, tena iko mbele yako, ambayo HUTAYAKUMBUKA mapito haya na changamoto zake. Kuna wengi wanashuhudia jinsi Bwana alivyowapitisha katika dhiki fulani, huenda hata wewe una ushuhuda ukiyakumbuka ya zamani.
Ni kazi ya shetani, kuvunja moyo na kutia Giza akili ili tusione Nuru kupitia ahadi za Mungu wetu. Hebu tumtazame Yesu aliye mwokozi wetu, kudumu kumpatia fadhaa zetu, naye ni mwaminifu, atatenda.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE NA AMANI MOYONI.
By. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210399.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***Bila kujali umejeruhiwa kiasi gani, bila kujali tatizo limedumu muda mrefu kiasi gani, bila kujali uzito wa tatizo lako, hata kama huoni mwisho wa shida yako. Hata ujione umeaibika na watu wanakubeza na dhihaka juu.
Neno la leo linasema, siku yaja, tena iko mbele yako, ambayo HUTAYAKUMBUKA mapito haya na changamoto zake. Kuna wengi wanashuhudia jinsi Bwana alivyowapitisha katika dhiki fulani, huenda hata wewe una ushuhuda ukiyakumbuka ya zamani.
Ni kazi ya shetani, kuvunja moyo na kutia Giza akili ili tusione Nuru kupitia ahadi za Mungu wetu. Hebu tumtazame Yesu aliye mwokozi wetu, kudumu kumpatia fadhaa zetu, naye ni mwaminifu, atatenda.
NAWATAKIA SIKU NJEMA YENYE BARAKA TELE NA AMANI MOYONI.
By. Eliezer Mwangosi
Simu: 0767210399.
0 comments:
Post a Comment