Wednesday, May 04, 2016

Linaweza lisiwe ni jina geni sana kwa msomaji wa habari hii, mzee Wilfred Jumanne Mwazini. Ni baba mzazi wa muimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili Samwel Mwazini, Jumapili hii amejipatia mke Bi. Petronila Asenga waliyekubaliana kuungana kwa njia ya ndoa takatifu kama mke na mume katika kanisa la Waadventista Wasabato Kongowe jijini Dar es Salaam.Ilikwa ni shangwe na nderemo katika viwanja vya kanisa hilo pale ambapo ndugu, jamaa, marafiki wa karibu wa familia hizo walipojitokeza kuwapongeza maharusi hawa kwa hatua hiyo kubwa katika maisha. Ni takribani miaka mitatu tangu tangu msiba wa mkewe ulipotokea mwaka 2013 mwezi wa 9 na hivyo kuiacha familia katika hali ya majonzi hadi ambapo Jumapili iliyopita familia ilikutana tena kwa ajili ya siku nzuri ya furaha kama hiyo. Timu nzima ya injilileo blog inatoa pongezi za dhati kwa familia nzima, ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo. TUNAWATAKIA MAISHA MAREFU YA NDOA NA BARAKA TELE.



****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA