Tuesday, May 03, 2016

Waefeso 3:20 "Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu."

Nakumbuka kisa cha kijana mmoja ambaye alipitia changamoto za maisha, akiwa ni msomi alyemaliza na kufaulu vizuri masomo ya chuo kikuu, lakini kwa bahati mbaya alikosa ajira. Zaidi ya miaka mitatu aliishi kwa kuomba misaada kwa watu huku akitegemea siku moja angepata kazi.

Katika hali ya kusikitisha, baada ya muda fulani kupita, alionekana hali imebadilika, anaongea peke yake barabarani na hakuwa na uwezo tena wa kiakili. Alipofanyiwa uchunguzi alionekana akili zimevurugika, kutokana na msongo wa mawazo. Mwisho ilibidi arudishwe kwao kijijini na ikawa ndio Mwisho wa ndoto za maisha yake.

Wewe na mimi tungali tunaishi hapa duniani, hatujawa salama kukutwa na hali kama hiyo, kutokana na sababu nyingine yoyote, tusipokuwa na elimu hii ya neno la Mungu. Tunashuhudia kila siku, vijana kwa wazee wakianza ulevi wa pombe au madawa, wengine tabia za kutoka nje ya ndoa au kusaliti wapenzi, ili kupoteza au kupunguza msongo wa mawazo. Mpendwa; Unawaza jambo gani kubwa? Ombi lako kuu la kila siku ni lipi?, kwake yote yanawezekana na zaidi.

Tunashuhudia watu wengi na hata wanaojiita watu wa Mungu, wakienda kwa waganga wa kienyeji japo kwa siri, kutafuta dawa za kutatua shida zao, na wengine ni kuhama kanisa hadi kanisa, nabii hadi nabii na mwisho wa yote anaambulia kufadhaika na kuvunjika moyo, japo wakati mwingine unaweza kujiona umefanikiwa kumbe mwisho wake ni majanga.

Neno la leo; linatuongoza kuona ufumbuzi wa changamoto zetu kupitia uweza wa Mungu. Lolote uliwazalo, bila kujali ni kubwa kiasi gani, na umeliombea kwa muda mrefu kiasi gani bila mafanikio, neno linasema; Mungu ANAWEZA KUFANYA ZAIDI YA HAYO. Tatizo kubwa ni mahusiano yetu na Mungu, wengi wanahitaji na kutamani Mungu awapatie mahitaji ya Mwili, lakini ndani ya mioyo yao hawako tayari kusalimisha maisha yao yatawaliwe na Mungu. HILO NI TATIZO KUBWA.

Mpendwa; neno linasema, yote na Zaidi yanawezekana ... "Kwa kadiri ya NGUVU itendayo kazi ndani yenu", siri kubwa ya mafanikio ni kuwa chini ya Uongozi wa Roho mtakatifu ambaye anaweza kukuvusha salama katika kila Dhoruba. Kutegemea akili zetu, waganga au mafundi, kutafuta sehemu ya kupoteza mawazo n.k, ni kujilisha upepo. Hata Manabii, wachungaji, mitume, wainjilisti nk, hatupaswi kuwatumainia, kila mtu binasi anapaswa kuishi katika nguvu na uweza wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu.

MUNGU BABA AWAJALIE WOTE NEEMA INAYOWEZA KUBADILI MAGUMU KUWA RAHISI NA ZAIDI YA MAHITAJI YENU.
NB: Usikose kusoma MADA za INJILI YA MILELE zinazoendelea kutolewa kwa ajili ya wito mkuu wa matengenezo kwa watoto wa Mungu kabla ya mlago wa Rehema kufungwa. 


Na. Ev. Eliezer Mwangosi.
Namba ya Simu: 0767 210 299 - Kwa ajili ya ushauri na maswali.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA