Tuesday, May 03, 2016

Katika hali isiyo ya kawaida sana kutokea, tumeshuhudia vitabu vya TUMAINI KUU vikigawiwa kwa wageni wote waliojitokeza kushuhudia ufungwaji ndoa Bw. Wilfred Jumanne Mwazini na Bi. Petronila Asenga katika kanisa la Waadventista Wasabato Kongowe la jijini Dar es Salaam.

Zoezi hilo lilianza mapema pale ambapo vitabu vilitolewa kwa mgeni mmoja mmoja hasa wale waliofika kutoa huduma katika harusi hiyo kama wapiga picha lakini baadaye mchungaji aliyekuwepo kwa ajili ya kufungisha ndoa aliposimama alianza kwa maneno mazuri ya kuonesha kutambua uwepo wa wageni wengi ambao sio waadventista na kisha kuwaomba wageni hao kusimama.

Baada ya tangazo hilo, kweli kulionekana kuwepo kwa wageni wengi, kisha alitoa wito kila mgeni kupewa kitabu, ndipo tulishuhudia maboksi yaliyokuwa na vitabu yakiletwa na wageni wote kupewa zawadi ya kitabu.

Zoezi hilo halikuishia ndani ya kanisa tu bali wagawaji walienda hadi nje na kumpatia kila mtu aliyekuwa akipita njia na yeyote aliyeonekana akishangaa tukio hilo.
Bwana Hussein Ijolo, alikuwa ni moja ya mgeni aliyepata kitabu
Bwana Abishua Mganga pia alipewa zawadi ya kitabu
Wageni akiwa wamesimama wakisubiri zawadi
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA