Thursday, June 09, 2016

Askofu Mkuu wa kanisa la Waadventista Wa Sabato Jimbo kuu la Kusini mwa Tanzani Mchungaji Mark Warwa Malekana
          Na mwandishi wetu, Dodoma
Ameyasema hayo mapema leo katika mkutano wa wanahabari na mawasiliano wa Tain ambapo alianza kwa utangulizi wa kusema nini maana SIKU ZA MWISHO.
Siku za mwisho zinaanza baada ya siku 1260 (538-1798) na akigusia tabia ya siku za mwisho Mchungaji Malekana alifafanua kwa kusoma Daniel 12:4 na siku hizo zinatabia kama;-
1. Watu wataenda mbali huku na huko 
2. Maarifa yataongezeka
Historia ya Dunia inaonesha kuwa teknolojia ilibadilika mara baada ya kalne ya 19 na mapinduzi ya viwanda yalibadilika na ilipiga hatua kwa kasi huku ikiongezeka.
Na leo kwa njia ya teknolojia ufahamu wa utaongezeka na hii huonekana wazi katika baadhi ya mafungu ya kitabu cha Daniel ikitaja maneno "Mabawa (uwepesi wa neno kwenda kwa kasi) na Sauti kuu (Injili ihubiriwe kwa nguvu zote)"
Mchungaji Malekana kwa kusisitiza somo hili alisema sasa ni wakati wa kurusha ujumbe wa kupaa kama neno mabawa lilivyotumika kwenye kitabu cha Biblia na kumalizia kwa kusema ni vyema washiriki kuvitumia vifaa vya teknolojia visivyoshikika(soft copy) na pia bila kusahau vitabu vinavyoshikika(Hard copy) hasa vitabu vitabu vya Biblia na Roho ya unabii.
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories: ,

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA