Monday, July 25, 2016

Sikukuu ya vibanda inayojulikana kama sherehe za makambi, ambazo hufanyika mara moja kwa mwaka, kwa mtaa wetu wa Kimara wenye makanisa mawili yaani King'ongo na Kimara yenyewe, makambi haya yamepata kufunguliwa rasmi 23 JULAI 2016 katika viwanja vya Kanisa la King'ongo lilipo Kimara DSM.
Mchungaji Jonas Singo mmoja wa wachungaji na wahudumu wa kambi hili alipata fursa ya kufungua kambi kwa kuvalishwa skafu na vijana wadogo watafuta njia na kisha alisoma maandiko na kusisitiza juu ya umuhimu ya kumtumikia Bwana pasipo kutoa udhuru.


Kikundi cha The Remnant Family walipokuwa wakihudumu siku ya ufunguzi wa makambi ya mtaa wa Kimara 2016.

Kwaya ya Tumaini toka kanisa la Kimara walihudumu pia katika Makambi mtaa wa Kimara 2016.
Hii ni kwaya ya King'ongo ambayo pia walihudumu kwenye kipindi cha uimbaji aiku ya ufunguzi wa Makambi ya mtaa wa Kimara 2016.

Kwaya ya Kanisa la Kimara Sda walipata fursa ya kuhudumu kwa njia ya uimbaji sku ya ufunguzi wa makambi ya mtaa wa Kimara 2016.
 Picha na habari kamili Bofya hapa KIMARA SDA WEBSITE
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA