Friday, July 29, 2016

Mchungaji na Mkurugenzi wa idara ya uwakili ya Konferensi ya Mashariki Kati mwa Tanzania ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato, Mchungaji Jonas Safiel Singo, alipata fursa ya kutoa huduma ya mahubiri nchini Marekani, pamoja na mambo mengine Mchungaji Singo alitoa huduma ya ubatizo na kubariki watoto nchini humo.
Pia siku ya Sabato ndani ya Kanisa la Maranatha Karibu SDA Church New Jersey Marekani alihubiri neno la Mungu lililokuwa limejikita kwenye mambo yafuatayo;-
  • Usikimbie matatizo yako yakabili kwa Jina Yesu
  • Mambo mengine huwezi kuyaepuka maishani
  • Usiogope kuanza upya maishani
  • Endeleza roho ya maombi na kubariki wengine
  • Shikilia roho ya kung'ang'ania ahadi za Bwana
Mchungaji Jonas Singo katika huduma nchini Marekani
Mchungaji Jonas Singo katika huduma nchini Marekani

Picha/Habari na Pr Jonas Singo

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA