Thursday, July 07, 2016

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla awapongeza kanisa la Waadventista Wasabato kwa shughuli za kijamii inazofanywa na kanisa hili. Baadhi ya Shughuli ambazo alizizungumzia ni pamoja na malezi ya vijana wadogo kwa wakubwa,kutoa misaada kwa wahitaji,kukemea matumizi ya madawa ya kulevya,uvutaji bangi, ukahaba na ushoga. Kupinga kwa nguvu mauwaji ya vikongwe na watu wenye ualibinizim. Aidha amewataka waumini na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanajiunga na bima ya afya kwaajili ya ulinzi wa afya zao. Katika kilele cha sherehe za jubilee ya miaka 50 ya utume jiji la Mwanza kanisa la Kirumba, Mh Hamisi Kigwangalla alipata nafasi ya kutembelea na kujionea jinsi huduma za afya zilivyokuwa zikitolewa bure kwa juma zima kwa wakazi wa Kirumba na viunga vyake, alitembelea mabanda ya maonesho ya kazi za mikono ya wajasiriamali wa kanisa hilo; pia alipata kutembelea jengo la Hospitali linalojengwa katika eneo la Pansiasi jijini Mwanza katika Makao makuu ya jimbo la South Nyanza Conference ya kanisa la Waadventista Wasabato. Miongoni mwa wageni waalikwa katika kilele cha sherehe hizi za jubilee ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Wilaya ya Ilemela Mh. Angelina Mabula.


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

2 comments:

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA