Sunday, August 21, 2016

Somo la Asubuhi linatoka katika kitabu cha MARANATHA, kitabu ambacho kinadhaminiwa na EGW Writtings maalumu kwa ajili ya Programu ya IBADA.
Maana njozi hii ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. Habakuki 2:3.
Imani iliyomtia nguvu Habakuki, watakatifu na wenye haki siku zile za majaribio magumu ni imani ile ile inayotunza watu wa Mungu leo. Katika nyakati zilizo na kiza kabisa, katika mazingira yasiyo mazuri kabisa, Mkristo muumini aweza kudumisha muunganiko kati ya roho yake na chanzo cha nuru na uwezo. Siku kwa siku, kwa njia ya imani kwa Mungu, tumaini lake na ujasiri vyaweza kufanywa upya tena.... Katika huduma kwa ajili ya Mungu hakutakuwa na kukata tamaa, kusitasita, wala hofu. Bwana atatimiza matarajio ya juu zaidi ya wale wawekao tegemeo lao kwake. Atawapa hekima inayohitajika kulingana na mahitaji yao mbalimbali.
Mtume Paulo anatoa ushuhuda juu ya uwepo wa mahitaji kwa wingi kwa ajili ya roho inayojaribiwa. Yeye alipewa uhakika wa kimbingu, “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.” Kwa shukrani na ujasiri mtumishi wa Mungu aliyejaribiwa aliitikia: “Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha na shida, kwa ajili ya Kristo. Kwa maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.” 2Kor. 12:9, 10.
Tunapaswa kuiendeleza na kuijenga imani ambayo manabii na mitume wameishuhudia - imani ambayo anakamata ahadi za Mungu na kusubiri ukombozi katika wakati aliouamuru na njia aliyoipanga. Neno la hakika la unabii Iitatimilika mwishoni katika ujio wenye utukufu wa Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo, kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. Wakati wa kusubiri waweza kuonekana kuwa mrefu, roho yaweza kuelemewa na matukio ya kukatisha tamaa, wengi ambao watu wamewaamini waweza kuanguka; lakini hebu tuungane na nabii aliyediriki kutia moyo Yuda wakati wa uasi mkubwa sana, kwa kusema, “. . .Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu: dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.”
Hebu daima tukumbuke ujumbe huu unaochangamsha, “Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. . . mwenye haki ataishi kwa imani yake.”
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA