Yesu alishuka kwenye mashua karibu na pwani ya Kapernaumu.
(tazama Marko 5) Wanafunzi wake bado walikuwa wamestushwa kutokana na
tukio la kukutana na mtu mwenye pepo huko Dekapoli. Kama kawaida, umati
wa watu ulikusanyika kumlaki. Wakiwa na shauku ya kutaka kumsikiliza,
watu katika umati ule walikuwa wakisukumana ili kuwa karibu Zaidi na
Yesu. Mara akaombwa msaada, wakati huu aliombwa msaada na wakuu wa
masinagogi.
Soma Marko 5:22-43 Wakati Yesu akiwa njiani kuelekea
kumhudumia kiongozi wa sinagogi kitu gani kilimzuia? Na ni kwa jinsi
gani alikabiliana na kizuizi hiko? Kitu cha muhimu hapa, Somo gani
tunapata hapa kulingana na kisa hiki, kuhusiana na kukabili kizuizi
unapokuwa katika kutoa huduma?
Hebu tukabiliane na hili, hakuna kati yetu anayependa
kukabiliana na vizuizi, sivyo? Tuna mambo mengi ya kufanya. Sehemu za
kwenda, na kazi zinazopaswa kufanyika. Tunaweka malengo kwa ajili yetu
na tunahitaji kufikia malengo hayo. Wakati mwingine tunahitaji kufikia
malengo hayo kwa muda Fulani tuliojiwekea, hata hivyo vizuizi vyaweza
kuingilia kati.
Ndiyo sababu, kama mtu anakuja na haja au ombi la kuhitaji
msaada, huweza kuonekana kama vile usumbufu hasa kama wakati sio
muafaka. Wakati mwingine unalazimika kutokuacha kile unacho kifanya kwa
wakati huo, Ni mara ngapi unapaswa kuacha hicho unachokifanya na kutoa
msaada lakini hufanyi hivyo kwasababu hutaki kufanya hivyo?
Hata hivyo mara kadhaa fursa kubwa za kuwahudumia watu
wengine mahitaji yao huja na vizuizi. Wengi tunajaribu kuvikwepa vizuizi
hivyo na tunasikitika pale mipango yetu inapofutika. Tunapo tazama
huduma ya Yesu tunagundua kwamba baadhi ya mahitaji, aliyoyajali mno
yalikuja na vizuizi na aliyashughulikia kwa upendo. Tunapofikiri kuhusu
hilo, fursa nyingi za kutoa huduma huja kwa njia ya vikwazo. Tumekwisha
kutazama kisa cha Msamaria mwema. Nani ajuaye alipokuwa anakwenda na
nini alikuwa anakwenda kufanya alipofika pale?, Hata hivyo alisimama na
kutoa huduma.
Zungumza juu ya vizuizi.
Mara ya mwisho ili kuwa lini, mtu alikukatiza akiwa na hitaji la kuomba msaada? Uliitikia vipi?****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment