Saturday, August 20, 2016

 
Sabato Mchana
Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili: Mk. 5:22–43, Mk. 10:46–52, Yn. 5:1–9, Zab. 139:1–13, Mk. 2:1–12, Mdo. 9:36–42.

Fungu la Kukariri: “‘Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina’” (Mathayo 9:35).

Mwanamke wa kiadventista katika moja ya nchi za kiafrika aliyekuwa amestaafu, hakua na nia ya kuacha kuhudumu baada ya kustaafu. Jamii yake ilihitaji huduma yake ya uponyaji kwasababu ya madhara yaliyo sababishwa na virusi vya UKIMWI. Msaada wa haraka ulikuwa unahitaji kwa watoto yatima ambao waliachwa na wazazi wao kutokana na ugonjwa wa UKIMWI ambao hawakupata lishe bora. Mwaka 2002, Yeye na kanisa lake walianza huduma ya kuwalisha watoto katika jamii inayowazunguka lishe bora kwa siku sita za juma. Walianza na watoto 50 na, kufikia 2012, walikua wakihudumia watoto 300 kwa siku. Iliyowapelekea wao kuanzisha shule ya awali na sasa watoto 45 kati yao wanahudhuria. Huduma nyingine ni pamoja na kusambaza nguo kutoa ADRA, Kugawa mboga mboga na mahindi kutoka bustani waliyokuwa wanaihudumia na kutunza wagonjwa, walianzisha mpango endelevu wa kukuza ujuzi kwaajili ya wanawake, ambapo walifundishana wao kwa wao ili kuendesha maisha yao. Hili linaelezea upendo wa Yesu ambao ulianzisha kanisa jipya. Mwanzoni kulikuwa na waumini watano, na ilipofikia mwaka 2012 walifikia watu 160. Mungu aliandaa njia kwaajili ya ujenzi wa jengo la watoto yatima na ujenzi wa jingo mpya la kanisa mwaka 2012.

Ni mfano wa nguvu kiasi gani wa utendaji, kufikia mahitaji ya jamii, ambayo ni muhimu sana kutendwa na wakristo.
Somo la Juma la hili limetafsiriwa na Naetwe Eliesa Kimweri na Agape P. Mrindoko.

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Categories:

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA