Somo la Asubuhi linatoka katika kitabu cha MARANATHA,
kitabu ambacho kinadhaminiwa na EGW Writtings maalumu kwa ajili ya
Programu ya IBADA.
Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti,...maana
kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.
Waebrania 11:5
Tunaishi katika kizazi kiovu. . . Kwa sababu ya kuongezeka
kwa maasi, upendo wa wengi unapungua. Henoko alitembea na Mungu kwa
miaka mia tatu. Nyakati hizi inaonekana kana kwamba muda kuwa mfupi, ni
sababu ya kufanya watu watafute kuwa wenye haki. Je, ni muhimu ya kwamba
vitisho vya ile siku ya Mungu viwekwe mbele yetu ili tuhimizwe kutenda
yaliyo sahihi? Kisa cha Henoko kinaletwa kwetu. Kwa mamia ya miaka
alitembea na Mungu. Hali akiishi katika kizazi potofu; kuchafuka kwa
maadili kulipozidi kumzunguka kila mahali; yeye alizoeza akili yake
kuabudu, na kupenda usafi. Mjadala wake ulijikita katika mambo ya
mbinguni. Aliielimisha akili yake ikimbie katika njia hii, na
alidhihirisha uwepo wa mapenzi ya uungu. . .
Henoko alikuwa na majaribu kama sisi. Alizingirwa na jamii
ambayo haikupatana na haki kama jinsi ilivyo kwetu leo. Hewa aliyovuta
ilikuwa imechafuliwa na dhambi na ufisadi, kama ilivyo yetu; na bado
aliishi maisha ya utakatifu. Hakuharibiwa na dhambi zilizotawala katika
kizazi aIichoish i kwacho. Vivyo hivyo twapaswa kusalia tukiwa safi na
bila kupotoshwa. Alikuwa mwakilishi wa watakatifu waishio kati ya hatari
kubwa na upotovu katika siku za mwisho. Kwa sababu ya uaminifu wake kwa
Mungu alibadilishwa. Vivyo hivyo, wanaosalia kuwa waaminifu, walio hai, watabadilishwa. “Heri wenye moyo safi: maana hao watamwona Mungu.” Kwa
miaka mia tatu Henoko alikuwa akitafuta usafi wa moyo, ili awe katika
mapatano na mbingu. Kwa karne tatu alikuwa ametembea na Mungu. Siku
baada ya siku alitamani ushirika wa karibu zaidi na Mungu; ushirika huu
uliendelea kuwaweka karibu zaidi na zaidi, hadi Mungu alipomchukua
kwake. Awali alikuwa amesimama katika kingo za ulimwengu unaadumu
milele, hatua moja tu kati yake na nchi ya waliobarikiwa; na kisha
malango yakafunguka, kule kutembea na Mungu ambako kwa muda mrefu
kulishafanyiwa mazoezi hapa duniani, kuliendelea, na akapita katika
malango haya na kuingia katika jiji takatifu, akiwa wa kwanza katika
wanadamu kuingia pale. . .
Mungu anatuita kuingia katika ushirika wa namna hiyo. Kama
ilivyokuwa tabia ya utakatifu ya Henoko, ndivyo ipaswavyo kuwa tabia ya
wale watakaokombolewa toka kati ya watu wakati wa kuja kwa Bwana mara ya
pili.****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
0 comments:
Post a Comment