Monday, August 22, 2016

Somo la Asubuhi linatoka katika kitabu cha MARANATHA, kitabu ambacho kinadhaminiwa na EGW Writtings maalumu kwa ajili ya Programu ya IBADA.
Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa. Isaya 26:21.

Kwa kasi na tena kwa uhakika hatia inakuja juu ya wakazi wa miji, kwa sababu ya kuongezeka kwa kudumu kwa uovu utendwao kwa makusudi. Ufisadi unaotawala, unazidi ule mwanadamu awezao kuuleza kwa maandishi. Kila siku inakuja pamoja na ufunuo mpya wa ugomvi, rushwa, na ulaghai; kila siku inakuja na taarifa za kutisha za vurugu na uvunjaji wa sheria, kutojali mahangaiko ya watu, udhalimu, maangamizi ya kikatiIi ya uhai wa watu.

Mungu wetu ni Mungu wa rehema. Kwa subira na huruma anadumu kushughulika na wavunja sheria. . . Mungu anawavumilia sana watu, na pia miji, huku akiendelea kwa rehema kutoa maonyo ili kuwaokoa kutoka katika ghadhabu yake; lakini wakati utakuja ambapo sauti yake ya kusihi itakoma. . .

Hali zinazoendelea katika jamii, hususan katika majiji makuu ya dunia, zinatangaza kwa sauti kubwa kama radi ya kwamba saa ya hukumu ya Mungu imekuja na kwamba mwisho wa mambo yote ya kidunia umekaribia. Tunasimama katika ukingo wa zahama ya karne zote. Kwa haraka zikifuatana hukumu za Mungu zitashuka - moto, mafuriko, matetemeko, pamoja na vita na umwagaji wa damu. . .

Dhoruba ya ghadhabu ya Mungu inajikusanya; na watakaopona ni wale tu watakaoukuwa wamepokea mwaliko wake wa rehema,... na kutakaswa kwa njia ya utii kwa sheria ya Mtawala wa mbinguni. Wenye haki pekee watafichwa pamoja na Kristo katika Mungu hadi uharibifu utakapokuwa umepita. Hebu lugha ya roho na iwe: 

“Ngome nyingine sina; nategemea kwako, Usinitupe Bwana, nipe neema yako, “Yafiche ubavuni Mwako maisha yangu; Nifishe bandarini, Wokoe moyo wangu!”

****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "KIFO" TOKA KWA PADACK

MAHUBIRI YA USHINDI HATIMAYE 2017 HAYA HAPA